Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 28 April 2015

NMB TABORA YATOA MSAADA MILIONI 25.


Na Hastin Liumba, TaboraBenk ya NMB Mihayo Tawi la Tabora imetoa msaada wa Computer na madawati 350 yenye thamani ya milioni 25.



Misaada hiyo ilitolewa katika shule tano zilizopo kwenye wilaya mbili za Uyui na  Tabora Manispaa.

Akikabidhi msaada huo mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa Lodovick Mwananzira, Menaja wa kanda Augustine Ibrahim alisema madawati hayo yatakuwa chachu kwa wanafunzi ambao walikuwa wanakaa sakafuni wakati wa masomo yao.

Alisema kila shule imepatia madawati  70 ambayo yanaweza kutumiwa na wanafunzi wapatao 210 kwa wastani,hivyo itasaidia kuondoa msongamano uliokuwa uliokuwa unawakabili wanafunzi hao kwa kukalia dawati moja ama kukaa sakafuni.

Alisema NMB kwa kutambua uwepo wa wateja wametenga kiasi cha milioni 50 kwa mwaka wa fedha 2015 ili kuweza kusaidia sekta ya afya na elimu mkoani tabora, kwani sekta hizo ni mhimu katika maisha ya binadamu.

Ibrahimu alisema kwa mwaka jana benki hiyo imetoa msaada wa bilioni 1.5 katika kusukama maendeleo kwenye wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ikiwa ni pamoja na wizara ya afya na kusadidia watu waliopata majanga pamoja na maafa mbalimbali.

Aidha alisema NMB inazadi kuboresha huduma yake ili kuweza kuwafikia wateja wake kwa urahisi ikiwa ni katika kuanzisha akaunti inayoitwa chapu chapu ambayo itamfikia mteja mahali popote atakapokuwa.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Lodovilick Mwananzira katika hafla fupi ya kupokea msaada huo iliyofanyika katika shule ya msingi mazoezi Mwenge iliyoko Tabora manispaa aliipongeza taasisi ya kibenki kwa kutambua umuhimu wa elimu.

 Alisema ili elimu iweze kuwa bora ni pale wanafunzi wanapopata vifaa vya kujifunzia na madawti ya kukalia wanapokuwa darasani hali hiyo humfanya mwanafunzi kujifunza kwa bidii na kupata msukoma hata wa kufanya vizuri katika mitihani yake.

Alisema ni jambo la kusikitisha saana kuona Mkoa wa tabora unakosa madawati katika shule wakati asilimia kubwa ya mbao zinazo zlishwa nchini zinatoka mkoani hapo huku akitoa wito kwa taasi mbali mbali zilizopo Mkoani hapo kuiga mfano bora kutoka Benki ya NMB Mihayo tawi la Tabora.

Hata hivyo amezitaka shule zilizopokea msaada huo wa madawati kuyatunza kama hadhina ya baadaye ikiwa ni pamoja na kuyafanyia marekebisho pale kunapo tokea hitarafu ili yaweza kutumika kizazai hadi vizazi.

No comments:

Post a Comment