Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 29 April 2015

CHUO CHA MUSOMA UTALII TABORA KUBORESHA MAFUNZO



Na Hastin Liumba, TaboraUONGOZI wa CHUO cha Musoma Utalii tawi la Tabora umesema utaendelea kutoa mafunzo ya elimu ya Utalii na Ualimu kadri ya maelekezo ya sera za nchi zinavyoelekeza.


Mkurugenzi wa chuo cha Musoma Utalii wa tawi hilo Shaban Mrutu alisema hayo kwenye mahafali ya 11 ya chuo hicho ambapo jumla ya wanachuo 197 walihitimu kozi mbalimbali.

Mrutu alisema chuo hicho kilianzishwa kwa madgumuni ya kukuza utalii nchini na sasa kimefikia mahali kimanzisha chuo cha Ualimu ambacho kitachukua wanafunzi zaidi ya 150 kwa wakati mmoja.

Alisema katika mahafali hayo kazi sita zimetoa wanafunzi 197 waliohitimu na kozi hizo ni Toursm and Hospitality,kozi ya Computer ICT na Secretarial.

Alitaja nyingine ni Nursery School Teaching, Journalism and Broadcasting na Record Management.

Alisema kozi hizo zimefundishwa kwa ufasaha na kwamba wahitimu ana mategemea makubwa watakuwa msaada mkubwa kwa jamii inayo wazunguka.

Aidha wahitimu pia wataingia kwenye soko la ajira la nchin wanachama wa afrila mashariki kwani mafunzo hayo yanatambulika kisheria.

Mkurugenzi huyo alisema pamoja na mazuri hayo pia chuo kimejipanga chini ya uongozi wake kusomesha wakufunzi wake ili waendane na hali ya ushindani iliyopo kwenye ajira.

Hata hivyo mkurugenzi huyo alibainisha chuo kuwa kina changamoto kadhaa ambazo ni upungufu wa vitabu vya Utalii,ukosefu wa maji safi na salama chuoni hapo kwani miundombinu yake bado.

Alitaja niyngine ni upatikanaji wa sehemu za kufanyia mazoezi kwa vitendo hasa kozi za Utalii na uandishi wa habari kwa njia ya utangazaji kwani haijaimarishwa.zinapatikana mbali na eneo la chuo.

No comments:

Post a Comment