Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 28 April 2015

WAZAZI TABORA WAASWA KUZINGATIA LISHE

Suala la lishe shuleni ni jambo la msingi sana

Na Hastin Liumba, TaboraWAZAZI mkoani Tabora wametakiwa  kuzingatia suala la kuwanyonyesha watoto wachanga kwani maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ili kuondokana na tatizo la udumavu wa ubongo na hadi sasa Tabora iko chini ya asilimia 20.


Mkurugenzi wa Taasisi ya chakula na lishe Dkt Jackline Kaganda alisema hayo katika kikao kazi kilichowahusisha Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Tabora,waganga wakuu wa Wilaya,na maafisa lishe wa kila wilaya.

Dk Kaganda alisema Tanzania inapambana na tatizo la udumavu wa ubongo ambapo mtoto aliyedumaa ubongo wake unakuwa na mafundo mafundo kwenye ubongo hivyo kushindwa kuchanganua mambo kwa urahisi.

Alisema wakurugenzi wahakikishe chumvi inayotumika ina madini joto ili kukabiliana na tatizo hilo na kuongeza kuwa katika Mikoa mingine kama Lindi nyumba chache tu ndizo zinazotumia chumvi yenye madini joto..


Nae Mwezeshaji katika kikao kazi hicho kutoka taasisi ya chakula na lishe Mwita Waibe alisema takwimu za kitaifa za mwaka 2010-2014 zinaonyesha kuwa watoto 2.7 milioni wamedumaa na asiliia 58 wapo kwenye Mikoa kumi ikiwemo Tabora.

Alisema pia unawaji wa mikono kwa maji safi na sabuni Mkoa wa Tabora upo chini ya asilimia moja huku unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee kwa miezi 6 ukiwa asilimia 45 tu,matumizi ya chumvi yenye madini joto ukiwa ni asilimia 40.

Waibe aliongeza kuwa upungufu wa damu ambao husababisha kuchoka sana na kusinzia kila mara pia hutokana na upungufu wa madini joto mwilini pamoja na ukosefu wa chakula dawa.

Kwa upande wake Katibu tawala wa Mkoa wa Tabora Kudra Mwinyimvua katika taarifa yake alisema ripoti ya Kitaifa ya tafiti ya lishe za afya 2010 inaonyesha watoto wenye umri kuanzia siku 0hadi miezi 59, wenye udumavu ni 33,upungufu wa wekundu wa damu 69,upungufu wa vitamin Asimia 33,upungufu wa madini joto 49

Katibu tawala huyo aliongeza pia wanawake walio katika umri wa kuzaa kuanzia miaka 15-49,wenye upungufu wa wekundu wa damu ni 55,upungufu wa madini ya joto 50,upungufu wa vitamin Asilimia 32 na kudai pia Halmashauri zote zinatekeleza usimamizi kuhakikisha chumvi zote zinazouzwa zina madini joto,ingawa dawa za kupimiamadini joto zinaletwa zikiwa zimeisha mda wake wa matumizi hivyo kushindwa kuendelea na upimaji.

No comments:

Post a Comment