Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 19 April 2015

AKUTWA AMECHINJWA, PIKIPIKI IKO PEMBENI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, ACP Jacob Mwaruanda

NA MWANDISHI WETU, SUMBAWANGA
CHARLES Kombe (28) mkazi wa Sumbawanga Asilia katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa na amekutwa amechinjwa pamoja na majeraha kichwani huku wauaji wakishindwa kuchukua chochote ikiwemo pikipiki yake iliyokutwa imeegeshwa eneo la tukio.


Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumapili Aprili 19, 2015 katika eneo la Uwanja wa Ndege mjini Sumbawanga.

Mwili wa marehemu uligunduliwa na watu waliokuwa wakipita njia katika uwanja huo wa ndege ambao waliukuta mwili huo ukiwa umelala kwenye majani huku pikipiki aliyokuwa nayo marehemu ikiwa imeegeshwa pembeni yake.

Mashuhuda walimeimbia www.brotherdanny5.blogspot.com kuwa walipokuwa wakielekea kusali alfajiri ambapo waliukuta mwili wa Charles ukiwa umelala pembezoni mwa barabara, pikipiki yake ikiwa imeegeshwa kama vile mtu ameiweka anasubiria kitu ikiwa imezimwa na funguo yake ikiwa imechomekwa kwenye sehemu yake.

Wamesema walipokagua eneo hilo walibaini damu sehemu za kichwani na simu yake ikiwa kwenye mfuko wa suruali ndipo wakapiga simu polisi kuwajulisha tukio hilo ambapo polisi walifika na kuichukua maiti kwa ajili ya kuifanyia uchunguzi na kuihifadhi katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa, mjini Sumbawanga.

Baba mdogo wa marehemu, Herman Kombe, amesema marehemu alikuwa hanywi pombe enzi za uhai wake na hakuwa na makundi ya mitaani zaidi ya kazi zake na kusali kila siku ambapo alikuwa mwanamaombi wa kikundi cha Charismatic cha Kanisa Katoliki.

Amesema enzi za uhai wake marehemu alikuwa akifanya kazi ya fundi redio katika kibanda kilichopo katika jengo la Ofisi ya CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini,kazi iliyomuweka karibu na wateja wengi ambao walimuamini.

Amesema jana Jumamosi kabla ya mauti kumfika alizungumza na marehemu wamtume mtu nyumbani kwao katika Kijiji cha Kirando wilayani humo kupeleka mahitaji ya familia kwa ajili ya kumalizia msiba wa dada yao aliyefariki katikati ya wiki iliyopita kwa kutumia pikipiki ya marehemu.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alipozungumza na www.brotherdanny5.blogspot.com kwa njia ya simu alikiri kupata taarifa za kifo na kueleza kuwa yeye na timu yake wanaifanyia kazi taarifa ili kuwasaka wauaji na kuwatia nguvuni ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki kwa mujibu  wa sheria za nchi.

“Tunaendelea na upelelezi wa kina ili kubaini waliofanya uhalifu huo kwa sababu mpaka sasa hatujapata taarifa sahihi ni nani aliyeshiriki kwenye kitendo hiki, tunaendelea na kazi tukikamilisha tutawapa taarifa na wala hatujakamata mtu yeyote mpaka sasa,” amesema.


No comments:

Post a Comment