Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 18 April 2015

RAIA WA BURUNDI WAANDAMANA DHIDI YA RAIS

Maandamano ya kumpinga rais wa Burundi Piere Nkurunziza yamefanyika mjini Bujumbura
Polisi nchini Burundi wamerusha mabomu ya kutoa machozi na maji, ili kuwatawanya mamia ya waandamanaji katika mji mkuu Bujumbura.

Maandamano hayo ni ya kumpinga Rais Pierre Nkurunziza, kutowania tena kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu ujao, unaopangiwa kufanyika mwezi Juni.
Mwaandishi wa BBC mjini Bujumbura, anasema kuwa malori makubwa yanayobeba vitoa machozi yamewekwa tayari kukabiliana na waandamanaji hao kote katika mji huo.
Anasema kuwa wazazi wamekimbia shuleni ili kuwaondosha watoto wao na kuwapeleka nyumbani.
Bwana Nkurunziza hajasema hadharani iwapo atawania kiti cha urais kwa muhula mwingine, lakini kuna tetesi kuwa ana mpango wa kufanya hivyo.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment