Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Monday, 20 April 2015
AFRIKA INALIA, DAMU INAMWAGWA NA WEUSI
Ndugu zangu,
Sote tunakumbuka mapambano yaliyoendeshwa na wazee wetu akina Autshumato, Langalibalele, Patrick Chamusso, Mosiuoa Lekota, Mac Maharaj, Michael Matsobane, Govan Mbeki, Sayed Adurohman Moturu, Walter Sisulu, Oliver Tambo, Nelson Mandela, Askofu Desmond Tutu, Kgalema Motlanthe na wengineo walivyopambana kuhusiana na utawala wa kibaguzi wa Makaburu licha ya uhuru walioupata kwa Waingereza Mei 31, 1910.
Mapambano hayo yaliwasababisha wazee wetu wengi kufa - wengine wakifia magerezani kwa mateso na kujaribu kutoroka kama Chief Maqoma, Maqana Nxele, Robert Sobukwe - wakatumikia miaka mingi katika kuhakikisha Mtu Mweusi anajikomboa kutoka kwenye minyororo ya ubaguzi wa rangi wa Makaburu.
Afrika ililia, wapenda amani na haki wakalia pamoja nayo mpaka mambo yalipokuwa shwari kuanzia mwaka 1987 wakati wa utawala wa Kaburu Pieter Willem Botha (maarufu kama Pik Botha) ambaye alianza kuwaachilia huru wafungwa mbalimbali wakiwemo Govan Mbeki baba yake rais wa zamani Thabo Mbeki na John Nkosi kabla ya kuachiliwa kwa Mandela mwaka 1990 baada ya kukaa gerezani kwa miaka 27 tangu alipohukumiwa kifungo cha maisha mwaka 1963.
Mateso waliyoyapata kwa ajili ya ardhi yao na watu wao hayamithiliki, na kwa hakika Waafrika wote tulikuwa nyuma yao na ndiyo maana mataifa mengi, hususan Tanzania, yaliamua kuwapa mafunzo wanaharakati na kusaidia kujikomboa.
Leo hii, watu wale wale ambao wenzao waliwasaidia kuwakomboa, wamegeuka na sasa ndio wanaoongoza kwa umwagaji wa damu. Wanawafyeka binadamu wenzao kwa ubaguzi - siyo wa rangi tu, bali mpaka wa utaifa.
Afrika Kusini imegeuka dimbwi la damu, utu umetoweka, umebakia unyama - tena hata Simba mwenye njaa anaweza kuwa na huruma!
Tunakwenda wapi jamani? Nani amewalaani hawa?
Tuombe kwa Mwenyezi Mungu aepushe janga hili, ambalo lisipofanyiwa kazi na kupatiwa ufumbuzi mapema, linaweza kuzua balaa kubwa zaidi.
MUNGU IBARIKI AFRIKA!
Ndugu yenu,
Daniel Mbega
Sumbawanga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment