Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 29 April 2015

BABA AUA MWANAYE MWANAFUNZI KWA KUMKUTA NA BARUA YA MAPENZI

 
IGP Ernest Mangu

NA WILLY SUMIA, SUMBAWANGA
GEOFFREY Robert Mwakatenya (15) anayesoma kidato cha pili katika shule ya sekondari Kilimani, Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, amepigwa hadi kufa na baba yake mzazi kwa kosa la kukutwa na barua ya mapenzi aliyomuandikia mpenzi wake.

Tukio hilo lilitokea Aprili 26, 2015 majira ya saa sita usiku katika Mtaa na Kata ya Majengo baada ya baba mzazi wa marehemu anayefahamika kwa jina la Robert Mwakatenya kufika nyumbani kwake na kumkuta mwanaye akiwa ameshika barua mkononi ambayo alibaini haikuwa ya kawaida.
Taarifa kutoka eneo la tukio zimedai kuwa baba huyo alianza kumhoji mwanaye ambapo katika hali ya kutubu alilazimika kueleza ukweli kuwa alikuwa amemuandikia binti ambaye ni mpenzi wake wa siku nyingi (jina linahifadhiwa) na wanawasiliana mara kwa mara.
Imeelezwa kuwa, baba alianza kumpiga mwanaye kwa mateke na fimbo sehemu mbali mbali za mwili na kusababisha kifo chake kabla ya kutoka nje ya nyumba na kutokomea kusikojulikana.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa bado jeshi la polisi halijafanikiwa kumkamata baba wa marehemu ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kamanda Mwaruanda aliomba ushirikiano kutoka kwa raia wema ili waweze kumtia nguvuni baba wa marehemu kutokana na unyama alioufanya kwa mwanaye wa kumzaa.
“Ni kweli tukio hilo lipo na tunaendelea na uchunguzi ili kuweza kumpata baba aliyefanya unyama kwa mtoto wake mwenyewe, tunawaomba wananchi watupe ushirikiano ili tuweze kumpata maana atakuwa amejificha sehemu walipo watu,” alisema.
Wimbi la wanafunzi wa shule za sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga kujiingiza katika mapenzi kabla ya wakati limekuwa kubwa ambapo wazazi wengi wamekuwa wakilalamikia watoto wao hasa wa kike kuwa na mahusiano ya mapenzi.
Kitengo cha Polisi Jamii mkoa wa Rukwa kimesema kumekuwepo na malalamiko mengi ya wazazi kuhusu watoto wa kike kuacha shule au kuwa watoro shuleni kutokana na wengi wao kushiriki katika mapenzi na wanaume ambao aidha ni wanafunzi wenzao au wasio wanafunzi.
Mpaka tunakwenda mitamboni, mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mazwi, Christina Sikazwe (17)  anatafutwa na wazazi wake kwa muda wa wiki tatu sasa hajulikani aliko ambapo hata shuleni haonekani ingawa taarifa kutoka ndani ya familia yake zinadai kuwa aliwahi kupotea kwa wiki mbili akapatikana kwa mwanamume mmoja.

No comments:

Post a Comment