Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 20 April 2015

WAKULIMA WA TUMBAKU WANG'AKA, TUMESAJILIWA KIHALALI!


Na Hastin Liumba, TaboraUMOJA wa wakulima wa kujetengemea wa zao la Tumbaku mkoani Tabora wasema umoja huo sio genge la wahuni bali wamejipanga kukomboa mkulima wa zao la Tumbaku Nchini.



Akizungumza wakati wa mkutano wa kupanga mikakati wa umoja huo katibu wake Ibrahimu Kisiliga alisema umoja  utahakikisha masoko yote ya tumbaku ambayo yanatarajiwa kufunguliwa Mei mwaka huu yanafunguliwa ,mkutano ambao uliofanyika kwenye hotel ya Manchester.

Alisema kwamba umoja huo umejipanga kuhakikisha kila soko linafanyika kwa wakati na sio kusubiria  vya ushirika vimalize kuunza kama inavyodaiwa na viongozi wao.

Alisema kwamba umoja huo upo kihalali na umesajiliwa na serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani na bodi ya tumbaku Tanzania ,hivyo basi kila soko wanahitaji kuunza zao kama ushirika mwengine wowote.

Alisema kwamba masoko yote ya tumbaku yafanyika kwa wakatio mmoja na vyama vya msingi vya ushirika ,ilikuweza kumaliza haraka masoko  iwe tofauti na mwaka huu ambapo wakulima wameuza mazao hadi Januari mwaka huu.

Naye mwenyekiti cha umoja huo Haruna Kapona alisema kwamba umoja huo umedharia kuhakikisha wakulima wanapata stahiki zao kama wakulima wengine na sio kubaguliwa na uongozi wa tumbaku mkoani hapa.

•Alisema kwamba ili kusiwepo na tatizo katika masoko wakulima wote wafunge tumbaku yao vizuri na wasiweke uchafu ili kufanya soko liwe bora kwa wakulima wa kujitegemea.

Hata hivyo umoja huo umewataka wanachama wao wote kupeleka tumbaku katika Magala ya kuhifadhi Tumbaku kwa ajili ya kusubiria masoko mara yatakapo anza.

Kapona alisema kwamba licha ya kupekeka mazao yao kwenye masoko lakini wahakikishe wanayalinda mabelo yao hadi watakapoyakabidhi kwenye kampuni ilinunua zao hilo.

No comments:

Post a Comment