National Arts Council BASATA
Tarehe: 24/04/2015
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
BASATA
Arts Centre Tel.
2863748/2860485
Fax: 0255- (022) – 286 0486
Ilala Sharif
Shamba
P.O. Box. 4779,
Dar es Salaam
E-mail:basata06@yahoo.com
KUSIMAMISHWA KWA SHINDANO LA UREMBO
LA MISS TANZANIA KWA MISIMU MIWILI KUKO PALEPALE
Katika
siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari na mitandao
mbalimbali ya kijamii kwamba shindano la urembo nchini maarufu kwa jina la Miss
Tanzania limefunguliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kwamba Kampuni
ya Lino International Agency LTD ambayo ni waendeshaji wa shindano hilo imewataka
mawakala wake kuanza maandalizi ya shindano hilo.
Taarifa
hizo za kufunguliwa shindano hilo zilienda mbali kwa kueleza kwamba mawakala
wametumiwa kalenda ya mashindano hayo kwa mwaka huu.
Baraza
linapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:
1. Wananchi
wapuuze taarifa hizo kwani kusimamishwa kwa shindano la Miss Tanzania bado kuko
palepale kama ilivyoelezwa katika barua ya BASATA ya tarehe 22/12/2014 waliyoandikiwa
Lino International Agency LTD ambayo pamoja na mambo mengine iliwataka
warekebishe kasoro kadhaa zilizojitokeza. Walisimamishwa kwa misimu miwili ya mwaka
2015 na 2016 ili kujipanga upya na kurekebisha kasoro husika.
2. BASATA
kama msimamizi na mratibu mkuu wa sekta ya Sanaa nchini ndilo lililolisimamisha
shindano hilo baada ya kubaini mapungufu mengi. Kusimamishwa kwa shindano hili
ilikuwa ni kwa njia ya kuufahamisha umma na kwa maana hiyo kama shindano
litafunguliwa njia hiyo-hiyo ya kutoa
taarifa kwa umma itatumika na si vinginevyo.
3. BASATA
linatoa wito kwa Lino International Agency LTD kutumia muda wake mwingi
kufanyia marekebisho mapungufu yaliyojitokeza ili mashindano haya yatakaporejea
yawe na mikakati na hadhi kuliko ilivyo sasa.
4. Aidha,
Baraza linawataka wasanii na wadau wote kuzingatia sheria, kanuni na taratibu
zilizopo katika kuendesha shughuli za Sanaa sambamba na kufuata mifumo sahihi
ya mawasiliano.
Sanaa
ni kazi, tuipende na kuithamini
Godfrey
Mngereza
KATIBU MTENDAJI
No comments:
Post a Comment