Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 20 April 2015

MCHUNGAJI ATANGAZA KUGOMBEA URAIS 2015

Na Rodrick Mushi, Moshi
MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Stephano Moshi (SMUCCO), Mchungaji Godfrey Malisa, ametangaza nia ya kugombea urais Oktoba mwaka huu kwa tikeki ya mgombea binafsi.

Mchungaji Malisa, alitangaza azma hiyo huku Serikali ikiwa bado haijaweka bayana kuwepo kwa mgombea binafsi kwa sababu Katiba Inayopendekezwa haijapitishwa.
Mwaka 2010, Malisa aligombea ubunge Jimbo la Moshi kwa tiketi ya Chama cha Tanzania Labour (TLP).
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Malisa alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuamini atachaguliwa.
Alisema ameamua kuchukua uamuzi huo ili kurejesha heshima ya taifa, kama ilivyokuwa imejengwa na na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Hata hivyo, alisema enzi za Mwalimu Nyerere lilikuwa na heshima kubwa ndani na nje ya nchi ambapo tangu kuondoka madarakani hajaweza kupatikana kiongozi wa kuvaa viatu vyake.
“Mimi nimeishi Marekani na China…taifa letu lilikuwa linaheshimika, leo hii hata amani imeanza kutoweka kutokana na maujai ya watu wenye ulemavu wa ngozi, ujambazi na wizi wa fedha za umma,” alisema.
Katika hatua nyingine, Malisa alisema Tanzania haipaswi kuitwa nchi masikini kwani ina rasilimali nyingi, lakini imekosa viongozi wa kuzilinda na kuzitumia kuinua uchumi wa taifa.
Alipoulizwa endapo nafasi ya mgombea binafsi haitakuwepo katika uchaguzi huo, alisema kama Katiba iliyopo haitafanyiwa marekebisho na kuwapo nafasi ya mgombea binafsi, atatangaza uamuzi mwingine.
CREDIT: MTANZANIA

No comments:

Post a Comment