Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 28 April 2015

6 WAKAMATWA NA VIPANDE 17 VYA MENO YA TEMBO


Hastin Liumba, TaboraJESHI la Polisi mkoani Tabora limefanikiwa kukamata watu sita wakiwa na vipande 17 vya meno ya tembo kutokana na operesheni maalumu.


Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi ACP Suzan Kaganda amesema watuhumiwa hao walikamatwa Aprili  18, 2015 majira ya saa 1.00 za jioni katika barabara ya Sikonge –Tabora jirani na benki ya CRDB tawi la Sikonge.

Alitaja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Baraka Yohana (29) mkazi wa Mnanira, Kigoma, Rashid Chande (28) mkazi wa Kizanga-Sikonge, Kenneth France kutoka Ofisi ya Mshauri wa Mgambo Manispaa ya Tabora, Ibrahimu John (25) mfanyabiashara Tabora, Peter Mollel (31) mfanyabiashara Tabora na Anthon Hamisi (42) mfanyabiashara Tabora.

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Noah yenye namba za usajili T 282 CXJ wakiwa na vipande hivyo 17 ambavyo ni sawa na meno 8 ya tembo.

 Kamanda alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na mara baada ya kukamilisha taratibu za upelelezi watafikishwa mahakamani mara moja.

Kamanda aliongeza kuwa katika msako huo unaoendelea mnamo  mwezi Aprili 13, 2015 majira ya saa 11.00 za jioni katika maeneo ya stendi ya mabasi wilayani Nzega mkoani Tabora pia walifanikiwa kukamata watu 3 waliokuwa na milipuko aina ya Power 90 ikiwa na uzito wa kilo 133 iliyokuwa ikisafirishwa kwa gari aina ya Toyota Saloon yenye namba T347 BFH inayofanya shughuli za taxi mjini Nzega.

Aliongeza kuwa watuhumiwa hao wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi na mara tu baada ya kukamilika upelelezi watafikishwamahakamani.


No comments:

Post a Comment