Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 4 August 2014

KESI YA WAANDISHI YAAHIRISHWA ETHIOPIA

Kesi ya wanablogu kumi waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya ugaidi imeahairishwa hadi Agosti 20.
Kesi hiyo ilianza leo miezi mitatu baada ya tisa kati yao kukamatwa na polisi.
Wanakabiliwa na mashitaka ya ugaidi chini ya sheria iliyoshutumiwa ya kupinga ugaidi.Mmoja wa wanablogu hao alishtakiwa bila kuwepo mahakamani.
Kesi hii imevutia hisia kubwa nje na ndani ya Ethiopia, hiyo basi hakukuwa na tofauti kubwa ilipoanza hivi leo.
Mahakama hiyo ilijazwa na raia wa Ethiopia, wanahabari hali kadhalika maafisa wa kidiplomasia. Wote walioshitakiwa walifika mahakamani. Mawakili walikuwa wamepinga kwa mapema mashitaka hayo wakisema kuwa hayakuwa na msingi.
Hata hivyo mahakama ilikataa kuwaachilia kwa dhamana wanablogu hao jinsi walivyokuwa wakitaka mawakili wao. Wote kumi wameshitakiwa kwa kubuni kikundi haramu vile vile kushirikiana na makundi ya upinzani yaliyopigwa marufuku ng’ambo na nchini.
Waendesha mashtaka walisema kuwa washtakiwa hao walipokea ufadhili na mafunzo ya kutengeneza vilipuzi.
Kitendo hicho cha kuwakamata wanablogu kimesababisha serikali ya Ethiopia kushutumiwa kimataifa na kutaja kuwa inatumia sheria dhidi ya ugaidi kukandamiza upinzani na uhuru wa vyombo vya habari nchini humo.

Katika mahojiano ya hivi majuzi na BBC waziri mkuu wa Ethiopia alikanusha madai ya kuwakandamiza wanahabari lakini akasema kuwa serikali haitawavumilia wanablogu na wanaharakati wanaonekana kushirikiana na makundi ya kigaidi nchini humo.
BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment