Watoto wa Wakimbizi kutoka Burundi wakiwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta ambapo wanahifadhiwa.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akizungumza
na uongozi na watendaji wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma alipofanya ziara
wilayani humo kwa ajili ya kukagua Kambi ya Nduta wilayani humo pamoja na Kambi
za Mtendeli na Karago wilayani Kakonko ambazo zipo katika maandalizi ya
kuwapokea wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa kwa muda katika Kambi ya Nyarugusu
mkaoni humo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Ruth Msafiri.
Mhandisi
wa Maji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Msafiri
Mtyaule akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mwamini Malemi (wa pili kulia) kuhusu kisima ambacho kitasambaza maji kwa
ajili ya wakimbizi kutoka Burundi ambao watahifadhiwa katika Kambi ya Mtendeli
wakitokea Kambi ya Nyarugusu ambapo wanahifadhiwa kwa muda.
Mkuu
wa Kambi ya Wakimbizi ya Nduta, Fred Nisajile akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wa pili kulia) moja wapo ya
madarasa yatakayotumiwa na wakimbizi watakaohamishiwa katika Kambi ya Karago
kutoka Kambi ya Nyarugusu wanapohifadhiwa kwa muda. Ubaoni ni picha na
maandishi yaliyoachwa na wakimbizi walioishi katika kambi hiyo kabla ya
kufungwa mwaka 2007.
Baadhi
ya Wakimbizi kutoka Burundi wakipokelewa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta. Idadi
ya wakimbizi kutoka nchini humo inazidi kuongezeka siku hadi siku.
Askari
Polisi wanaosimamia usalama katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wakikagua mizigo
ya wakimbizi kutoka Burundi wanaopokelewa katika kambi hiyo ili kuhakikisha
usalama wa mizigo yao.
Baadhi
ya mahema yanayojengwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo
mkoani Kigoma ambayo yatatumika kuwahifadhi wakimbizi kutoka Burundi
wanaoendelea kuwahamishiwa kambini hapo kutoka Kambi ya Nyarugusu ambapo
walikuwa wamehifadhiwa kwa muda.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment