Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 18 October 2015

MAGUFULI ASHIRIKI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU FILIKUNJOMBE NA WENZAKE WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA HELIKOPTA


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli  akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa(CCM) Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta juzi katika pori la akiba la mbuga ya Selous. Marehemu aliagwa katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.PICHA NA MICHUZI JR.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimfariji Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
 Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe akilia kwa uchungu kufuatia kifo cha Mumwe Deo Filikunjombe,wakati wa kuaga katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
 Dkt Magufuli akifarijiana na Mh.Zitto Kabwe  wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
 Dkt Magufuli alishindwa kujizuia kutoa machozi ya huzuni  wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
 Majeneza yenye miili ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deogratias Filikunjombe na ndugu zake, Plasdus Ngabuma na Casablanga Haule yakiwa yamewekwa mbele ya waombolezaji  wakati wa kuaga katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. kabla ya kusafirishwa kwenda Ludewa kwa mazishi mkoani Njombe.

No comments:

Post a Comment