Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 23 October 2015

MAOFISA WA TAASISI YA STEP1 YA KOREA WAPATA MAFUNZO YA UENDESHAJI MITAMBO TBL


 Meneja wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Bw. Calvin Martin (wa pili kushoto), akiwaonyesha Watafiti kutoka Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojkia na wageni kutoka Taasisi ya STEPI ya Korea, mitambo mipya ya kuzalisha bia, walipotembelea kiwanda hicho, Dar es Salaam kujifunza kuhusu uendeshaji na aina ya mitambo.

 Maofisa kutoka Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wageni wao kutoka Taasisi ya STEPI ya Korea wakimsikiliza kwa makini, Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw Calvin Martin )wa pili kulia), walipofika kiwandani hapo Dar es Salaam jana kujifunza kuhusu uendeshaji wa kiwanda, aina ya mitambo na ushirikiano na taasisi zingine. Kulia ni Meneja Usalama wa TBL, Bw. Renatus Nyanda.
 Maofisa wa TBL, Wizara ya Mawasiliano, Teknolojia na Sayansi wakiwa katika picha ya pamoja
 Mkuu wa Kitengo cha Utafiti Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Rafael Kibunda (kulia), Mtafiti kutoka Wizara hiyo, Profesa Rogers Msuya (kushoto) na Maofisa kutoka Taasisi ya STEPI ya Korea, wakimsikiliza kwa makini, Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Calvin Martin, walipotembelea kiwanda hicho Dar es Salaam jana kwa ajili ya kujifunza kuhusu uendeshaji wa mitambo. (Na Mpigapicha Wetu)
Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Calvin Martin (aliyenyoosha mikono), akifafanua jambo, wakati akiwatembeza maofisa kutoka WIzara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mkuu wa Kitengo cha Utafiti, Profesa Rafael Kibunda (wa pili kushoto), Mtafiti Profesa Rogers Msuya (Kulia) na Profesa Hyunho Kim (kushoto), kutoka Taasisi ya STEPI ya Korea.

No comments:

Post a Comment