Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 18 October 2015

MGOMBEA WA CCM MANONGA ASWEKWA RUMANDE

 Mgombea Ubunge wa jimbo la Manonga (kushoto) Ally Nguzo akiwa na mhanga aliyeshambuliwa na mgombea ubunge wa jimbo hilo Seif Gulamali (CCM) kulia Mkuraba Makala mara baada ya kutoka hospitali.
Mhanga aliyeshambuliwa na mgombea ubunge jimbo la Manonga Seif Gulamali (CCM) akionyesha moja ya majeraha yake kwa mwandishi wa habari.

Na Mwandishi Wetu, Igunga
JESHI la Polisi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora limemkamata na kumshikilia kwa masaa mawili mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Manonga Seif Gulamali kwa tuhuma za kushambulia raia mmoja kwa mabapa ya mapanga akiwa na wenzake na kumsababishia majeraha.



Akiongea na mwandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Hamis Issa alisema licha ya kupokea taarifa kadhaa za vurugu na fujo katika baadhi ya majimbo bado tukio la Igunga halijamfikia mezani licha kupewa taarifa na uongozi wa CHADEMA mkoa juu ya tukio hilo.

Kamanda huyo alisema atalifuatlia tukio hilo kwa ukaribu ili vurugu zaidi zisiendelee zaidi na upelelezi wake unaendelea.

Hata hivyo waandishi walipotafuta nini kilijiri katika tukio hilo kwa kamanda wa polisi (OCD) wilaya ya Igunga Abed Maige alikiri ni kweli walimkamata mgombea wa CCM Seif Gulamali kwa kwa tuhuma za shambulio hilo.

OCD Maige alisema mgombea huyo wa CCM alikamatwa siku ya Ijumaa majiraya saa nne asubuhi na aliachiwa kwa dhamana majira ya saa sita mchana na upelelezi watukio hilo unaendelea.

Kwa ufupi alisema walipokea taarifa toka kituo kidogo cha Kata ya Ziba kuwa Gulamali na wenzake kadhaa wameshambulia mtu kwa bapa za mapanga na kusababisha majeraha kwa Mkuraba Ngumi Makala (33) mkazi wa kata ya Iborogero.

Gazeti hili lilimtafuta mhanga wa tukio hilo na kufanikiwa kumkuta nyumbani kwake Iborogelo baada ya kuruhusiwa kutoka Kituo cha Afya Ziba kumkuta na majeraha usoni mbavuni na kidoleni.

Makala kwamasikitikoalisemaakiwabandanikwakenabiashara zake majira ya saa 03:30 usiku ghafla aliona gari mojalikija kwakasi huku likiwalimewasha taa kali na lilisimama mbele ya banda lake.

Alisema ghalfa walishuka vijana watatu wakiwa na mapanga na watu hao mmoja alimzaba kibao na wakaanza kusemayeye anajifanya ni CHADEMA sana sasa leo atakoma.

Akiwa anashangaa ghafla alipigwa panga sehemu ya jicho la kushoto na alidondoka chini na watu haowalianza kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake.

Alisema wakati yupochini akishambuliwa alimtambua mgombea wa CCM jimbo la Manonga Seif Gulamali aliteremka ndani ya gari na kijana mmoja  na kuanza kushusha bendera za CHADEMA na kuchana picha za Lowassa namgombea ubunge Ally Nguzo.

“Kamahaitoshi watu hao ambao nikiwaona nitawatambua walibomoa banda langu la biashara likaanguka banda ambalo nimekuwa nikifanya  biashara ya mbogamboga,viungo na mkaa,” alisema Makala.

Alisema baada ya uharamia wao dereva aliingia ndani ya gari nakupiga honi ambapo walimacha hapo chini nakuingia kwenye gari na kuondoka.

Makala alisema alipiga kelele za kuombamsaada nawananchi walijitokeza kumsaidia hadi kituocha polisi ambapo alipewa PF 3 na kwenda hospitali.

Aidha kesho yake walikuja askari polisi toka kituo cha polisi Igunga na walimhoji na waliondoka hadi aliposikiakuwa amekamatwa na kuwekwa ndani kwa saa kadhaa.

Gazeti hili lilimtafuta Seif Gulamali kuelezea mkasa huo hakupatikana na simu zake zilikuwa zimezmwa huku taarifa nyingine zikisemayupo kata ya Nguru akiendelea nakampeni zake.

Taarifa zaidi zinasema kamati ya ulinzi na usalama siku Jumamosi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nane mchana kujadili Jimbo la Manonga na vurugu zinazoendelea.

No comments:

Post a Comment