Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Friday, 23 October 2015
MGOMBEA CHADEMA AKOSWA RISASI
Na Mwandishi Wetu, Igunga
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Manonga wilayani Igunga kupitia Chadema, Ally Khalfan Nguzo, anadaiwa kukoswa risasi wakati wakati akitokea kwenye mkutano wa kampeni.
Mwenyekiti Chadema Jimbo la Manonga, Joram Makala, amesema tukio hilo lilitokea Septemba 6, mwaka huu wakitokea kwenye kampeni za mgombea ubunge jimbo la Manonga Ally Khalfan Nguzo kjiji cha Bulumbela Kata ya Ziba saa 07:36 usiku gari lao namba T 464 BKB lilipigwa risasi kioo cha mbele.
Alisema tukio hilo bahati nzuri risasi hiyo haikumpata mtu na msafara huo uliamua kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa za shambulio hilo.
Mgombea ubunge jimbo la Manonga Ally Nguzo alikiri ni kweli alikoswa risasi nataarifa zilitolewa polisi na kwamba risasi hiyo ilipigwa toka msituni majira ya jioni akitoka kwenye kampeni na bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa.
Taarifa zinasema, kampeni katika jimbo hilo zimekuwa kama za uahasama, ambapo hata wachimbaji wadogo wadogo wa madini ya dhahabu Kijiji cha Ikombandulu namba sita na namba mbili Kata ya Mwashiku wilayani Igunga wanadai wamekuwa wakitishiwa maisha kwa muda mrefu wasijiunge na CHADEMA kwani watahamishwa kwenye machimbo hayo.
Wakiongea kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea ubunge Jimbo la Manonga kwa tiketi ya CHADEMA ambaye anaungwa mkono na umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) Ally Khalfan Nguzo walisema wamechoshwa na vitisho hivyo kwani wanaona wanadhalilishwa.
“Tumekuwa tukiambiwa na viongozi wa CCM tukiweka bendera ama mabango ya CHADEMA ni za hatari kwa maisha yao na wataleta vita hivyo hakuna sababu ya wao kuweka bendera hizo,” walisema.
Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Manonga Joramu J Makala alisema mgombea ubunge jimbo la Manonga kwa tiketi ya CCM anawatisha wananchi kwamba wakichagua CHADEMA watahatarisha amani ya jimbo na nchi.
Aidha alisema CCM wamekuwa wakitumia sungusungu kuwatisha wananchi kwamba yoyote ambaye ataonyesha kuunga mkono CHADEMA au kutundika bendera mabango atashughulikiwa.
Alisema kijiji hicho kina madini na kwamba mgombea wa CCM Seif Gulamali amekuwa akizunguka nyakati za usiku saa nane kutisha watu huku akiomba kadi za kupigia kura na kuwaeleza atawapatia mikopo kazi ambayo amekuwa akiifanya na kwa kushirikiana na mabalozi wa CCM.
Alisema mwenyekiti wa kijiji kwa tiketi ya CHADEMA Emmanuel Mipawa na mwenyekiti wa kitongoji cha Choma Emmanuel Maswira walipigwa na mgombea ubunge wa CCM akiwa anatekeleza majukumu yake ya kampeni hata hivyo hawakutaka makuu waliamua kumuachia Mungu.
Asha Salumu Khalfan alilieleza gazeti hili kuwa alitishiwa maisha akiwa anatekeleza majukumu yake kama mgombea ubunge viti maalumu jimbo la Manonga kwa tiketi ya CUF.
Alisema wakati yuko kwenye pikipiki alirushiwa mawe huku akitukanwa matusi ya nguoni na wafuasi wa CCM kwa kuwa anahamasisha wananchi kujiunga na CHADEMA amakupigia chama hicho kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Alisema matukio mengine ni wafuasi wa CCM wanaoaminika ni Green Guard walifika kijiji cha Chibiso kata ya Choma na kuamuru wakazi wa eneo hilo kushusha bendera za CHADEMA huku wakitoa maneno ya kashfa na matuzi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment