Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (kulia), Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kutengeneza Magari ya ASHOK LEYLAND ya nchini India, Bhimasena Rau wakisaini Mkataba wa ununuzi wa magari kwa ajili ya matumizi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambavyo ni Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (kulia), Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kutengeneza Magari ya ASHOK LEYLAND ya nchini India, Bhimasena Rau wakipongezana baada ya kusaini Mkataba wa ununuzi wa magari kwa ajili ya matumizi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambavyo ni Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (watatu kushoto), akitoa neno la shukrani baada ya kusaini mkataba wa ununuzi wa magari ya Kampuni ya ASHOK LEYLAND ya nchini India. Magari hayo ni kwa ajili ya matumizi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Jumanne Sagini, wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kulia) akipokea Mkataba wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Watumishi wa Jeshi la Magereza kutoka kwa Makamu wa Rais wa Kampuni ya Ujenzi ya Poly Technologies ya nchini China. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja. Halfa hiyo ilifanyika katika Ukumbi mdogo wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (katikati aliyevaa tai), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wakumi kulia), Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Jumanne Sagini (wanane kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Viongozi wa Kampuni ya Kutengeneza Magari ya ASHOK LEYLAND ya nchini India. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Serikali
ya Tanzania imeingia Mkataba wa ununuzi wa magari kwa Vyombo vya Ulinzi na
Usalama nchini na Kampuni ya Motorrama (T) LTD ambayo ni Wakala wa Magari aina
ya ASHOK LEYLAND kutoka nchini India.
Mkataba
huo umesaniwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job
Masima pamoja na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo ya Utengenezaji wa magari,
Bhimasena Rau ukishuhudiwa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika
Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
mara baada mkataba huo kusainiwa, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John
Casmir Minja aliishukuru Serikali kwa msaada huo ambao utasaidia kutatua tatizo
la uhaba wa magari katika Jeshi la Magereza.
“Utekelezaji
wa mpango huu katika Jeshi la Magereza utakuwa na manufaa makubwa kwani
utapunguza tatizo la uhaba wa magari kwa ajili ya shughuli za uendeshaji na
utawala pamoja na utekelezaji wa jukumu la kuwasafirisha Mahabusu kwenda
mahakamani na kurudi magerezani,” alisema Minja.
Lengo kubwa la ununuzi wa Magari hayo unalenga
kuboresha huduma za usafiri pamoja na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa
majukumu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa nchini.
No comments:
Post a Comment