Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 23 October 2015

KAMATI YA STARS YATOA NAMBA ZA UCHANGIAJI

Katibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda (kulia) akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) kuhusu kuichangia timu hiyo. Kushoto ni Ofisa Habari Mawasiliano na Habari wa TFF, Baraka Kizuguto.
Katibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda leo amefanya makutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume, ambapo ametumia nafasi hiyo kutangaza namba za simu za uchangiaji kwa Watanzania kwa ajili ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Akiongea na waandishi wa habari, Teddy amesema watanzania wanaweza kuichangia Taifa Stars kiasi chochote cha fedha kuanzia shilingi mia moja (TZS 100) kwenda namba 0654-888868 (Tigo Pesa) na 0789-530668 (Airtel Money) ambazo zitatumika kwa ajili ya motisha kwa wachezaji, uhamasishaji/masoko na maboresho ya kambi za ndani na nje ya nchi.
Aidha Teddy amesema Kamati ya Taifa Stars inaandaa utaratibu kwa ajili ya washabiki watakaotaka kusafiri kuelekea nchini Algeria katika mchezo wa marudiano, waweze kuchangia gharama za usafiri ili waweze kwenda kuipa sapoti Stars katika mchezo wa marudaiano Novemba 17, 2015.
“KamatI inaendelea na mchakato wa kukamilisha suala la kambi ya Taifa Stars, na mpaka sasa tunasubiri majibu kutoka katika vyama vya soka vya vya nchi tunazotaka kuweka kambi ambazo ni Afrika Kusini, Dubai na Oman kabla ya kutangaza rasmi kambi itakapokuwa” Alisema Teddy.
Kamati inawaomba watanzania, wadau, washabiki na wapenzi wa mpira miguu nchini kuichangia timu ya Taifa kupitia namba zilizotolewa na pia kujitokeza kwa wingi kuujaza uwanja wa Taifa siku ya mchezo wa tarehe 14 Novemba, 2015

No comments:

Post a Comment