Prashant alikuwa amepelekwa na kuwekwa chumba cha kuhifadhia maiti kimakosa
Mwanamume aliyeshangaza wahudumu wa mochari nchini India kwa kuamka muda mfupi kabla ya kufanyiwa upasuaji amefariki.
Mwanamume huyo kwa jina Prashant, alifariki siku mbili baadaye akitibiwa katika hospitali inayomiliki chumba hicho cha kuhifadhia maiti.
Prashant, 50, ambaye hakuwa na makao, aligonga vichwa vya habari alipoamka baada yake kutangazwa kuwa alikuwa amefariki na daktari mkuu wa hospitali moja mjini Mumbai.
Alipelekwa mara moja hadi kwenye ufuo, licha ya kanuni za hospitali kusema mtu aliyefariki anafaa kukaa kwenye wadi saa mbili kuthibitisha ni kweli amefariki.
Haijabainika ni nini kilichomuua.
Mwili wake ulifanyiwa upasuaji baadaye Jumatano.
Dkt Suleman Merchant, mkuu wa hospitali ya manispaa ya Lokmanya Tilak amesema Prashant, alifariki Jumanne usiku.
"Alikuwa akitibiwa kwa kuwa na mabuu kwenye sikio lake la kulia na alikuwa amepoteza fahamu. Aidha, aliongezewa damu kwa sababu alikuwa akiugua anaemia,” aliongeza.
Awali, madaktari walisema alipofikishwa hospitalini mara ya kwanza Jumapili, mwili wake ulikuwa na matatizo ya kuendesha shughuli muhimu na pia alikuwa akiropokwa.
Alipelekwa hospitalini baada ya kupatikana akiwa amepoteza fahamu katika kituo kimoja cha mabasi.
Dkt Merchant amesema uchunguzi unafanywa kubaini kulifanyika nini hadi Prashant akapelekwa ufuoni moja kwa moja baada ya daktari kusema alikuwa amefariki mara ya kwanza.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment