Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Saturday 24 October 2015
DED IGUNGA AELEZEA MAELEKEZO YA NEC
Na Hastin Liumba, Tabora
MKURUGENZI wa halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora na msimamizi wa uchaguzijmbo la Manonga na Igunga Rustika Turuka ametoa ufafanuzi wa maekelezomapya ya uchaguzi.
Akiongea na gazeti hili mkurugenzi huyo alitoa ufafanuzi mpya uliotolewa na tume ya taifa ya uchaguzi ya taifa (NEC) ambao alisema umepokelewa na ofisi yake kama maagizo kupitia barua pepe.
Alibainisha kuwa maelekezo hayo yanasema katika kichwa cha habari kisemacho maelekezo ya nyongeza kuhusu upigaji kura yanasema mpiga kura ambaye atakuwa na kadi ya mpiga kura ila namba yake ni tofauti na iliyo kwenye daftari la kituo ataruhusiwa kupiga kura.
Aidha aliongeza wapiga kura ambaopicha zao hazionekanani vizuri au hazionekani kabisa kwenye daftari lakudumu la wapiga kura wataruhusiwa kupiga kura.
Alitaja maelekezo mengine ni wapiga kura walioandikishwa na tume na wanaishi katika maeneo mapya ya kiutawala yaliyogaanywa wakati au baada ya zoezi la uandikishwaji kukamilika hivyo majina hayo kutofautiana na majina yaliyopo kwenye kadi zao wataruhusiwa kupiga kura.
Turuka anaongeza wapiga kura ambao hawaonekanai kwenye mfumo wa daftari lakini wana vitambulisho vilivyotolewa na tume na fomu zao za kuandikishwa kufikishwa tume namajina yao kuandaliwa katika katika mfumo wa orodha bila picha na kupelekwa vituo walivyojiandikisha ,hivyo mpiga kura asiye na kadi wataruhusiwa kupiga kura.
Msimamizi huyo anaongeza maagizo na maelekezo hayo yanasema kwa mujibu wa sharia mpiga kura ni lazima awe na kadi ndio aruhusiwe kupiga kura,hivyo mpiga kura asiye na kadi hataruhusiwa kupiga kura.
Aidha alisema kipengele cha mwisho alisema wapiga kura ambao wanakadi ya kupigia kura lakini hawamo katika daftari la kudumu la wapiga kura la kudumu kituoni hataruhusiwa kupiga kura.
Mkurugenzi na msimamizi huyo alisema maelekezo hayo yametolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mwezi oktoba 23,2015 kwa njia ya barua pepe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment