Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 17 October 2015

ACT-WAZALENDO YAMLILIA DEO FILIKUNJOMBE


            
TAARIFA KWA UMMA

KWA Masikitiko makubwa na kwa niaba ya chama, napenda kutuma salaam za rambirambi kwa familia ya Deo Haule Filikunjombe, Ofisi ya Bunge, Chama cha Mapinduzi(CCM) na Taifa kwa ujumla kufuatia kifo cha ghafla kisichotarajiwa cha  Ndugu yetu na rafiki yetu Marehemu Deo Filikunjombe.

Kwa  yakini kifo cha Deo Filikunjombe kimeiumiza zaidi ACT-Wazalendo huenda kuliko hata CCM yenyewe! Deo Haule Filikunjombe kwetu  alikuwa rafiki namba moja wa ACT-Wazalendo, ingawa wengi wanamfahamu kama rafiki wa karibu wa Ndugu Zitto Zuberi Kabwe, ambaye ndiye Kiongozi wa Chama.
Kwetu Deo Filikunjombe alikuwa ni zaidi ya rafiki na kwa lugha rahisio zaidi tulimtambua kama mwanachama hai wa ACT Wazalendo asiye na kadi.
Tunatambua Mchango wake wa hali na mali katika  kushauriana nae kuhusu kuanzisha chama kipya Cha Siasa ambacho sasa ni Chama Mbadala cha Upinzani kinachotambuliwa kwa jina la ACT-Wazalendo
. Kama rafiki wa karibu alitutia moyo sote kwamba tunaweza kuanzisha chama kingine na kikaja kuwa mbadala wa kweli, Alikuwa mshauri, mchangiaji mawazo na mchangiaji namba moja wa raslimali katika kuendesha chama chetu.
Deo ametutoka tukiwa bado tunamuhitaji sana, akiwa bado anahitajika na chama chake CCM, akiwa bado sana sana anahitajika na wananchi wake wa Ludewa, akiwa bado mno atahitajiwa na ofisi ya bunge lakini yote kwa yote, familia ilimhitaji zaidi.
Ameondoka Deo, lakini historia ya taifa letu itamuenzi kama historia ya chama chetu, chama chake cha CCM na Bunge la Jamhuri ya Muungano zitakavyomuenzi.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe


___________________________________________________________
        203 Mpakani A Street, Kijiitonyama,  P.O. Box 105043,  Dar es salaam.
Tel: +255 22 277 1103, Mob: +255 763 463740 / +255 715 784670,
 Email: acttanzania@gmail.com Website: www.act.or.tz

Maingu Samson Mwigamba,
         KATIBU MKUU.

No comments:

Post a Comment