Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Sunday 18 October 2015
WANANCHI JIMBO LA MANONGA AHADI ZA CCM HAZITEKELEZEKI - NGUZO
Na Hastin Liumba, NkingaWANANCHI wa kata ya Nkinga jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora wameelezwa ni wahanga wa maisha bora kwa kila Mtanzania waliyoahidiwa kwamiaka kumi ya utawala wa CCM.
Ally Khalfan Nguzo mgombea wa (CHADEMA) anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) alisema hayo katika viwanja vya soko la kata ya Nkinga.
Nguzo alisema katika kipindi cha miaka 53 sasa CCM iko madarakani na zaidi mwaka 2010 chama hicho kilikuja na kaulimbiu ya maisha bora kwa kila Mtanzania lakini leo tunashuhudia hali mbaya ya uchumi wa Tanzania na hasa maisha ya watanzania kuishi maisha duni.
Mgombea huyo alisema hali za watu hasa wananchi jimbo la Manonga hasa Kata ya Nkinga walivyopigika na maisha.
Alisema CCM wamekuwa wakibeza ilani yetu wakisema haitekelezeki hebu tuangalie ilani yao kama leo ndani ya miaka kumi kama imetekelezeka zaidi ya maumivu ya Watanzania.
Alisema zipo sababu kadhaa ambazo zinasababisha Watanzania kuwa masikini ambazo moja ya sababu hizo katiba mbaya ya Nchi ambayo haina maslahi kwa wananchi.
Aidha alisema kingine ni siasa ya nchi hii inavyotumika kuwa ni sehemu ya kukuza uchumi huku watalaam wakipuuzwa.
Nguzo alitaja kingine ni ukiritimba wa CCM ambao hadi sasa wanaamini na kutekeleza kazi zao kwa hisia za chama kimoja.
Alisema haya ni mambo ambayo CCM wamekuwa wakipitia humo ili kutuangamiza Watanzania.
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Joseph Kashindye akiongea na wananchi hao aliwaeleza wasidanganyike na ahadi za CCM kuwa kila kijiji kitapatiwa sh milioni 50.
Kashindye alisema huo ni uongo kwani fedha hiyo haipo na kwamba fedha ya serikali haiwezi kupelekwa kwa wananchi kama ya dukani ama mtu binafsi.
Alisema hata kama fedha hiyo itakuwepo ni dhahiri itaanzia ngazi ya halmashauri ama manispaa na majiji ndipo imfike mwananchi wa kawaida na zitakuwa ni fedha za maendeleo ambazo ukizigawanya zitabaki kiduchu ni uzushi tu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment