Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 18 October 2015

WATU WANNE WANAOMPINGA DENIS SASSOU NGUESSO WAUAWA CONGO

Maandamano yameanza nchini Congo kupinga hatua ya rais wa nchi hiyo Denis Sassou Nguesso kuwania muhula wa tatu
Maandamano yameanza nchini Congo kupinga hatua ya rais wa nchi hiyo Denis Sassou Nguesso kuwania muhula wa tatu.

Polisi wa kukabiliana na fujo nchini humo wamefyatua mabomu ya kutoa machozi na risasi wakijaribu kuvunja maandamano hayo.
Takriban watu wanne wameripotiwa kuuawa katika makabiliano hayo katika mji mkuu wa Congo Pointe-Noire.
Maandamano hayo yameibuka huku ikiwa imesalia mwezi mmoja tu kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni ya kuamua iwapo taifa hilo litafutilia mbali kipengee cha katiba kinachomzuia rais wa taifa hilo kuongoza kwa zaidi ya mihula miwili.
Aidha raia wataamua iwapo rais atakayeongoza taifa hilo anastahili kuwa amezidi umri wa miaka 70 au la.
Rais Sassou Nguesso ana umri wa miaka 72 na kikatiba haruhusiwi kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao kwani amekuwa uongozini kwa zaidi ya awamu mbili.
Ametawala nchi hiyo kwa zaidi ya miaka thelathini sasa.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment