Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani), wakati wa mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Wizara hiyo,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Mabibi na Mabwana,
Kama
mnavyojua tarehe 25 ya mwezi huu wa Oktoba mwaka 2015 siku ya Jumapili katika
nchi yetu kutafanyika Uchaguzi Mkuu kwa ajili ya
kuchagua rais, wabunge na madiwani zoezi ambalo litawashirikisha
watanzania wote waliojiandikisha kupiga kura kwa mujibu wa sheria.
Zoezi
hili kwa mujibu wa sheria za uchaguzi litasimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
yaani NEC kama ambavyo imekuwa ikifanyika katika chaguzi mbalimbali zilizopita
ama kuwahi kufanyika katika nchi yetu.
Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi inalo jukumu kubwa la kuhakikisha ulinzi na usalama
wa raia na mali zao unaimarishwa kabla, wakati na baada ya zoezi hilo la
Uchaguzi Mkuu katika maeneo yote ya nchi yetu, ili wananchi waweze kuwa salama
na kuendelea na maisha yao ya kila siku.
Ndugu
Waandishi wa habari,
Kumekuwepo na taarifa mbalimbali za vitisho
zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na hata mitaani na watu wasio na nia
njema kwa taifa letu, zikiwataka
wananchi wanunue mahitaji yao mbalimbali ikiwemo vyakula na kuvihifadhi kwa
ajili ya kuja kuvitumia wakati na baada ya uchaguzi kwa ubashiri wa kuwepo kwa
vurugu wakati ama baada ya uchaguzi.
Taarifa
hizi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na mitaani kwa ujumla ni taarifa
potofu ambazo zinalenga kuwajengea wananchi hofu na mashaka, wasiwasi na
vitisho pasipo sababu zozote zenye tija kwa taifa
letu.
Ndugu
zangu Waandishi wa habari,
Nitoe rai kwa Raia wote waishio hapa nchini yaani Watanzania
na Wageni kupuuza taarifa zote zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na
mitaani kwa kuwa taarifa hizo si za kweli, na wala hazilengi kulinda amani
iliyopo nchini kwetu.
Pamoja
na hayo kumekuwa na matamko kwa baadhi ya wanasiasa katika kampeni zao kudai kuwa
Serikali itasitisha posho za askari mara baada ya Uchaguzi Mkuu, Taarifa hizi si za kweli kwani Posho za
Vyombo vyote vya dola vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi ni za kudumu kama ilivyoelekezwa
katika waraka wetu, hazitafutwa wala kubadilika na iwapo zitabadilika ni kwa
kupandishwa na wala si kufutwa.
Nawaomba
wananchi wote watii sheria za nchi na
zile za Tume ya Uchaguzi zinazoongoza
Uchaguzi Mkuu sambamba na kufuata Maelekezo yatakayotolewa na Tume hiyo kabla,
wakati na baada ya kupiga kura jambo litakalosaidia kuilinda amani ya nchi yetu,
kwani kila Mtanzania anao wajibu wa kuilinda amani kwa kufuata sheria za nchi
bila kushurutishwa.
Wananchi
wanapaswa kutambua kuwa baada ya uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka
huu maisha ya watanzania yanapaswa kuendelea kama kawaida hivyo itikadi zao za
vyama vya siasa zisiwatofautishe na kuwajengea chuki, uhasama ama uadui kwani
watanzania ni wamoja na wamekuwa wakiishi kwa amani, umoja na ushirikiano
katika kuendeleza taifa hili.
Ndugu
waandishi wa Habari,
Wananchi hawapaswi kuwa na hofu yoyote kwa kuwa Serikali ya
awamu ya nne ambayo imeongoza na kuwatumikia wananchi kwa kipindi cha miaka
kumi inakusudia kwa dhati kukabidhi
madaraka kwa serikali iyajo ya awamu ya tano katika hali ya amani na utulivu.
Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama
inawahakikishia wananchi kuwa itahakikisha hali ya amani na utulivu inakuwepo
na kuimarishwa kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu mpaka pale ambapo
Uongozi wa serikali ya awamu ya tano utakapoingia madarakani.
Wananchi
watoe taarifa Polisi pale watakapoona
kuna dalili za uvunjifu wa amani
kwa kupiga simu ya bure namba 112.
Nawashukuru
kwa kunisikiliza, Asanteni .
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment