Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 18 October 2015

PAPA FRANCIS AWEKA HISTORIA

Papa Francis
Historia ya kanisa katoliki inatarajiwa kuandikishwa upya leo na Papa Francis huko Vatican.

Kivipi labda umejiuliza?
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis anatarajiwa kuwatawaza mume na mke kuwa watakatifu.
Louis na Zelie Martin walikuwa wapenzi waloishi katika karne 19.
Image captionLouis na Zelie Martin walikuwa wapenzi waloishi katika karne 19.
Wawili hao walifanikiwa kuwapata watoto 9, japo wanne waliaga dunia wakiwa bado wachanga.
Watano waliojaliwa kuishi hadi kuwa watu wazima waliishia kuwa watawa wote.
Mdogo zaidi kati yao ndiye aliyepata umaarufu zaidi na alifahamika kwa jina la Theresa kutoka Lisiex.
Image copyrightAFP
Image captionShughuli hii ya leo itafanyika katika ukumbi wa kanisa hilo huko Vatican ambapo mkutano wa viongozi wa kidini au makadinali unaendelea.
Theresa alisifiwa kwa maisha yake ya ukristo akitawazwa kuwa mtakatifu mwaka wa 1925.
Shughuli hii ya leo itafanyika katika ukumbi wa kanisa hilo huko Vatican ambapo mkutano wa viongozi wa kidini au makadinali unaendelea.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment