Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu Tanzania kutoka Umoja wa Afrika (AU), Rais wa Zamani wa Msumbiji, Mhe Armando Emilio Guebuza. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (Katikati kulia) akimfafanulia jambo Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu Tanzania kutoka Umoja wa Afrika (AU), Rais wa Zamani wa Msumbiji, Mhe Armando Emilio Guebuza (wapili kushoto), pamoja na wajumbe wenzake, jinsi Tanzania ilivyojipanga kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu utakavyokuwa wa amani. Wakwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Timu ya
Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu Tanzania kutoka Umoja wa Afrika (AU), ambaye pia ni
Rais wa Zamani wa Msumbiji, Armando Emilio Guebuza (kulia) akimfafanulia jambo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) wakati Mkuu huyo
pamoja na wajumbe wenzake walipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake kwa
lengo la kujadili masuala mbalimbali ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika
Oktoba 25 mwaka huu, hata hivyo, Chikawe aliwahakikishia kuwa Uchaguzi huo
utakuwa wa amani. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak
Abdulwakil. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
*****************************************************************
No comments:
Post a Comment