Dk.
Umanath Nayak, mshauri mkuu wa magonjwa ya saratani ya kichwa na shingo
pamoja na upasuaji kwa njia ya roboti katika hospitali ya saratani ya
Apollo Hyderabad nchini India.
Na Mwandishi Wetu
Sekta ya afya duniani imeshuhudia mapinduzi
yanayolenga kuongeza umri wa kuishi, ubora wa maisha, njia mbadala za uchunguzi,
njia bora za matibabu, na pia ufanisi na ubora katika huduma za afya. Teknohama
imekuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo ya ndani ya sekta hii muhimu. Makampuni
yanayohusika na kutengeneza vifaa vya tiba hivi sasa yanalenga katika
kutengeneza roboti ambazo hufanya upasuaji kwa ufanisi zaidi bila madhara
makubwa kwa mgonjwa.
Kuna
matumaini sana katika upasuaji kwa kutumia teknolojia ya Roboti. Teknolojia hii
ni ishara ya mapinduzi katika sekta ya afya, na ni moja ya mambo muhimu
yanayoongelewa sana katika upasuaji hivi leo. Mfumo wa upasuaji kwa kutumia
roboti umeletwa ili kusaidia katika upasuaji mgumu, ambao hufanyika kwa shida,
au unaohusisha maeneo ambayo ni magumu kufikika na hatari. Kwa kutumia mikono maalumu
inayopatikana katika Roboti hilo upasuaji huo urahisishwa zaidi.
Mikono ya Roboti hudhibitiwa na kompyuta
inayoendeshwa na mpasuaji kwa kutumia mikono na miguu. Udhibiti huu ni sawa na ule
wa mchezo wa video, maarufu kama ‘video game’ ambao huwezesha upatikanaji kwa
usahihi zaidi wa maeneo magumu kufikika ikilinganishwa na njia iliyokuwa
ikitumika awali ya ‘laparoscopic’.
Kutumia matundu madogo sana, upasuaji wa aina hii unaweza kuondoa uvimbe
uliojificha pasipo uharibifu wa tishu na pia humsaidia mgonjwa kutokaa
hospitalini muda mrefu pamoja kupona ndani ya muda mfupi. Teknolojia hii
inapunguza hatari ya uharibifu wa mishipa na tishu katika eneo husika.
Upasuaji kwa kutumia Roboti unaweza kutumika kutibu
hali mbalimbali kama vile magonjwa ya kina mama (gynaecologic), ikiwa ni pamoja
kuondoa mfuko wa uzazi (hysterectomy), kutibu maambukizi kwenye leya ya ndani
katika mfuko wa uzazi (endometriosis), uvimbe kwenye mfuko wa uzazi (fibroids
uterine), saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya mfuko wa kizazi, fistula na
viungo katika nyonga kutoka nje (pelvic organ prolapsed). Utaratibu wa upasuaji
na ushonaji unaweza kufanyika kwa usahihi zaidi kupitia teknolojia hii.
Kulingana na huduma ya afya inayoitajika na umri wa mgonjwa, upasuaji kutumia
Roboti pia unaweza kusaidia kuboresha afya ya uzazi na kumsaidia mgonjwa uwezo
wa kuzaa.
Kwa wagonjwa wa saratani, mara nyingi upasuaji wa aina
hii huusisha upasuaji wa kichwa, shingo,
ulimi, tezi dume, magonjwa ya wanawake, kuondoa uvimbe kwenye utumbo
(colorectal surgery) na upasuaji unaohusisha nyonga.
Mfumo huu wa upasuaji una msaada mkubwa kwa wagonjwa
ambao wanahitaji upasuaji wa tezi upasuaji unaohusisha kuchana sehemu ya chini
ya shingo. Kwa kutumia roboti sasa inawezekana kufanya upasuaji wa tezi bila
kuchana shingo kwa sehemu kubwa na bila kuacha kovu inayoonekana.
Dk Umanath
Nayak, mshauri mkuu wa wa magonjwa ya saratani ya kichwa na shingo pamoja na upasuaji
kwa njia ya roboti kutoka hospitali ya saratani ya Apollo Hyderabad India ameelezea
faida ya upasuaji kwa kutumia Roboti. Anasema kuwa, "teknolojia ya kutumia Robot katika upasuaji itadumu sana kama
tunaweza kuona faida nyingi za teknolojia hii ikilinganishwa na njia mbalimbali
za zamani za upasuaji. Ni hatua ya pili ya upasuaji kwa kutumia mashine maalumu
huku ukiangalia kwenye Skrini ya computer (laparoscopic). Hii itapunguza haja
ya kufanya upasuaji wa wazi kwa wagonjwa wenye matatizo ya uzazi "
Anaongeza
kuwa, "Upasuaji wa kutumia Robot ni
njia mpya ya upasuaji ya isiyo na madhara na inajumuisha upasuaji wa kawaida
(Open surgery) na Upasuaji wa kutumia skrini ya computer (laparoscopic). Kwa
msaada wa Mikono maalumu ya Robot inayodhibitiwa, daktari anaweza kufanya
upasuaji kupitia mikato midogo sana. Teknolojia hii husababisha kutokuwa na
makovu makubwa yatokanayo na kukatwa sana, kutokuwepo na upungufu wa damu,
maumivu baada ya upasuaji na kupona kwa haraka zaidi ".
Aidha mtaalamu
wa magonjwa ya saratani nchini Dk. Harrison Chuwa, anasema kuwa “upasuaji kwa
njia ya roboti ni njia kuu ya kufanya upasuaji ambayo itapunguza mapungufu ya
kibinadamu na hata kovu la operesheni kuwa dogo ambalo aliweze kufanya mwili
wako kuonekana tofauti na ulivyokuwa awali. Faida nyingine ya upasuaji kwa njia
ya roboti ni kwamba unahitaji rasimali kidogo ya binadamu ili kufanikisha kazi
hii.
Teknolojia ya
roboti haipatikani nchini Tanzania, lakini watanzania wengi wanasumbuliwa na saratani
za kichwa na shingo na mfumo wa mkojo (mfano. kibofu), uzazi, upasuaji wa
utumbo mkubwa, na matatizo mengine wamepata huduma hii mara kadhaa pale
walipopata rufaa ya kwenda kutibiwa katika hospitali za Apollo nchini India.
Ishara
nyingine nyingi bado zina mjadala kwa maana njia hii ni mpya tokea upasuaji wa
laparoscopic uanzishwe. Muda unavyosogea, upasuaji kwa njia ya roboti
unatarajiwa kuchukua nafasi za upasuaji wa kawaida wa saratani na utakuwa ni
msaada na kimbilio kwa wengi wanaoteseka na saratani na mapungufu mengine. Inaweza tokea siku hapo baadae wakati daktari
wa upasuaji amekaa ofisini kwake na anamfanyia mgonjwa operesheni au upasuaji
akiwa mbali kwa msaada wa mfumo wa roboti.
Mwaka jana, Hospitali Apollo mjini Apollo Chennai na Hyderabad
imefanikiwa kufanya upasuaji mfululizo wa tezi kupitia teknolojia hii. Hakuna
shaka kwamba upasuaji wa kutumia Robot ni kifaa muhimu katika masuala ya
upasuaji, mchango huu muhimu unajidhihirisha hata katika nchi zinazoendelea.
Kuhusu Hospitali ya
Apollo
Hospitali
za Apollo ni za kwanza katika eneo Asia Pacific kutoa huduma za upasuaji kwa
kutumia mfumo huu wa Robot, ambayo ni aina ya upasuaji isiyokuwa na madhara.
Taasisi ya upasuaji kutumia Robot iliyopo hospitalini hapo wamejitoa kipekee
katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
Taasisi
ina wataalamu waliobobea kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo katika utoaji wa
huduma vifaa vya matibabu vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu bora kwa mgonjwa.
Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa Robot ya Da Vinci inayotumika katika upasuaji.
Mfumo huu wa
upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa magonjwa yanayohusiana na
mfumo wa mkojo (Urology), magonjwa ya wanawake (Gynaecology), moyo, utumbo, na
magonjwa ya watoto na matatizo ya uti wa mgongo.
No comments:
Post a Comment