Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 18 October 2015

WAWILI MBARONI KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA MIWILI

Hasira imetanda New Delhi baada ya mtoto wa miaka 2 kubakwa India
Polisi mjini Delhi, India wamewakamata vijana wawili, wanaotuhumiwa kwa ubakaji wa mtoto wa miaka mwili.

Kisa hicho cha ubakaji ni mojawapo wa visa vinavyoendelea mjini humo na kueneza mshtuko mkubwa duniani.
Vijana hao walio na umri wa miaka 17 walitiwa nguvuni baada ya polisi kuwahoji wenyeji wa kijiji kulikotokea tukio hilo la ubakaji.
Image copyrightEPA
Image captionHasira imetokana na serikali kushindwa kutunga sheria mpya itakayowalinda wanawake na watoto wa kike India
Mkuu wa mawaziri mjini Delhi Arvind Kejriwal ameshtumu serikali kuu ya India kwa kushindwa kuweka sera za kukabiliana na dhulma dhidi ya watoto.
Kumetibuka hasira miongoni mwa wenyeji na haswa wanawake baada ya tukio lingine ambapo kitoto cha miaka miwili kilibakwa na kutupwa kwenye bustani huku akivuja damu.
Wakati huohuo,wanaume wengine 5 wametiwa mbaroni kwa tuhuma za ubakaji wa mtoto mwenye umri wa miaka 5 pekee.
Tukio hilo la pili katika mji mkuu wa India New Delhi lilitokea katika maeneo ya mashariki mwa Delhi.
Image copyrightap
Image captionMji mkuu wa Delhi umeshuhudia matukio 2000 ya ubakaji katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Watoto hao walidanganywa na pipi wakaingia katika nyumba ya jirani yao kabla ya kubakwa.
Kwa sasa watoto hao wanapokea matibabu maalum na wanaendelea kupata nafuu kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika.
Matukio hayo yameibua hasira miongoni mwa wenyeji na hofu miongoni mwa wanawake ambao wana watoto wa kike.
Mji mkuu wa Delhi umeshuhudia matukio 2000 ya ubakaji katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment