Mkuu wa chama tawala cha India, cha BJP Amit Shah, amewalaumu wanasiasa wanne wa chama hicho kwa kutoa matamshi ya kutatanisha kuhusu ng'ombe na nyama ya mnyama huyo.
Mmoja alitaka hukumu ya kifo, kwa watu wanaochinja ng'ombe; na mwengine alitoa maanani kisa ambapo Muislamu, aliyetuhumiwa kula nyama ya ng'ombe, alichapwa mikwaju na kundi la watu.
Alidunisha tukio hilo akisema kuwa hiyo ilikuwa ni ajali tu.
Katika kipindi cha mwezi juma lilopita, vifo vingine viwili vya Waislamu, vilihusishwa na ghasia za wazalendo wa Kihindu, kuhusu ng'ombe na ulaji wa nyama ya ng'ombe.
Mapema leo dereva mmoja katika jimbo la Kashmir aliaga dunia kufuatia majeraha aliyopata gari lake lilipowashwa moto
Wahindu ndio wengi zaidi katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu wanaoamini na kuabudu mnyama Ng'ombe.
Kinaya ni kuwa wengi wao pamoja na waislamu na wakristu walio wachache hula nyama ya ng'ombe.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment