Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 18 October 2015

KERRY KUKUTANA NA VIONGOZI WA ISRAEL NA PALESTINA

John kerry kujadili ghasia zilizozuka upya baina ya WaIsraili na WaPalestina.
Waziri wa Mashauri ya nchi za nje wa Marekani, John Kerry, atakutana na waziri mkuu wa Israil, Benjamin Netanyahu juma hili, huko Ujerumani, kujadili ghasia zilizozuka baina ya WaIsraili na WaPalestina.

Bwana Kerry amesema atakutana pia na kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas.
Image copyrightReuters
Image captionTangazo hilo limekuja wakati jeshi la Israil limewaondoa waumini kadha wa Kiyahudi
Tangazo hilo limekuja wakati jeshi la Israil limewaondoa waumini kadha wa Kiyahudi, ambao polisi wanasema, waliingia kinyume cha sheria, katika madhabahu ya kidini katika ufukwe wa Magharibi unaokaliwa na Israeli.
Kundi la WaIsraili 30, lilikwenda kwenye kaburi la Joseph, huko Nablus leo alfajiri, na kuzusha mapambano dhidi ya Wa-Palestina.
Image copyrightReuters
Image captionWimbi jipya la ghasia limesababisha vifo vya wa Israili 8, na zaidi ya WaPalestina 40
Kaburi hilo lilichomwa na Wa-Palestina siku ya Ijumaa.
Wa-Palestina wanne waliuwawa jana, wakishukiwa kuwa waliwashambulia ama walinuia kuwashambulia waIsraili kwa visu.
Wimbi jipya la ghasia limesababisha vifo vya wa Israili 8, na zaidi ya WaPalestina 40, katika majuma ya karibuni.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment