Chancellor Merkel wa Ujerumani
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel yuko Uturuki kwa ziara mahsusi ya kujadili uhamiaji na wakimbizi na rais na waziri mkuu wa nchi hiyo.
Mzozo wa wahamiaji unatarajiwa kuwa mada kuu ikiwa haitakuwa ndiyo ajenda ya ziara hiyo Ankara.
Bi Merkel anaitaka Uturuki iimarishe mipaka yake na mataifa ya jumuia ya bara Ulaya, ili kukomesha msafara wa wakimbizi wanaomiminika kuelekea Ujerumani.
Aidha umoja wa ulaya ulikuwa umetoa mapendekezo ya kutaka Uturuki iwasaidie kukabiliana na idadi kubwa ya wahamiaji na wakimbizi wanaomiminika na kuingia barani humo.
Ili kuafikia azimio lao, viongozi wakuu wa bara hilo wataipa Uturuki fedha na viza ya bure kwa raia wake, kuzuru bara Ulaya bila masharti yeyote ilimradi tu itafunga mpaka wake.
Mwandishi wa BBC huko Berlin, anasema kuwa Bi Merkel yuko katika nafasi ngumu mno.
Kiongozi huyo wa Ujerumani amekuwa katika mstari wa mbele wa kukataa kata kata Uturuki isijiunge na muungano wa bara ulaya EU.
Hata hivyo sasa anahitaji kwa dharura msaada wa taifa hilo kuzima uhamiaji wa wakimbizi raia wa Syria wanaotokea Uturuki.
Aidha Bi Merkel amelaumiwa kwa kupuuza ukiukaji wa haki za kibinadamu nchini Uturuki.
Ziara yake imesadifiana na ripoti kuwa vikosi vya polisi vimewakamata watu 50 mjini Instabul kutokana na madai kuwa walikuwa na uhusiano na wapiganaji wa Islamic State.
Magazeti nchini humo yameripoti kuwa asilimia kubwa ya watu waliokamatwa ni raia wa kigeni waliokuwa na mipango ya kuelekea katika maeneo ya mapigano nchini Syria na Iraq.
Waziri mkuu Ahmet Davutoglu ameilaumu kundi la IS kwa milipuko miwili iliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 100 mjini Ankara juma lililopita.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment