TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA
Mnamo
mwezi wa Machi 2014 Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilipokea taarifa
kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu ugonjwa wa Ebola katika nchi
za Afrika Magharibi ambao ulianzia katika ya Guinea na kusambaa katika
nchi za Siera Leone, Liberia na Nigeria. Hadi tarehe 31 Julai, 2014
idadi ya wagonjwa ilikuwa 1323 na vifo 729.
Ugonjwa
wa Ebola husababishwa na virusi vya Ebola. Dalili zake ni homa kali ya
ghafla, kulegea mwili, maumivu ya misuli, kuuma kichwa, na vidonda
kooni. Mara nyingi dalili hizo hufuatiwa na kutapika, kuharisha, vipele
vya ngozi, figo na ini kushindwa kufanya kazi na kwa baadhi ya wagonjwa
kutokwa damu ndani na nje mwilini. Kipindi cha kuonekana kwa dalili za
ugonjwa ni kati ya siku 2 hadi 21 baada ya kupata maambukizi.
Ugonjwa wa Ebola unaambukiza kwa kasi na unaenea kati ya mtu na mtu kwa:-
kugusa damu na majimaji kutoka mwilini mwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo
kugusa maiti wakati ya mtu aliyekufa kwa ugonjwa huu.
kugusa wanyama walioambukizwa Mizoga na wazima kama vile sokwe na swala wa msitu.
Aidha Ugonjwa wa Ebola hauna tiba wala chanjo.
Hadi sasa hapa nchini Tanzania hakuna mgonjwa yoyote aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa virusi vya Ebola.
Wizara
ya Afya na ustawi wa Jamii imeandaa mikakati ya kuzuia ugojnwa huu
usiingie hapa nchini na ikiwa utaiingia uweze kudhibitiwa kabla
haujasambaa. Mikakati hiyo ni pamoja na:
Kuunda
kikosi kazi (Task Force) kinachohusisha wajumbe mbalimbali wakiwemo
wadau wa maendeleo ikiwa ni pamoja na WHO, UNICEF, USAID na CDC kwa
ajili ya kuweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huu ikwa ni pamoja na
kusimamia utekelezaji wa mpango wa dharura wa kukabiliana na Ebola
ambao tayari umeandaliwa.
Kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Makatibu Tawala na Waganga Wakuu wote wa Mikoa.
Aidha
taarifa hii pia imejumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa
(Ainisho la Ugonjwa), “Fact sheet” ya ugonjwa, Mwongozo kwa watumishi wa
afya wa namna ya kuchukua sampuli, na na namna ya kuwahudumia
wagonjwa.
Kuboresha ufuatiliaji na utambuzi wa
ugonjwa katika maeneo ya viwanja vya ndege na mipakani ili kuweza
kubaini wasafiri watakaoonyesha dalili za ugonjwa au wenye viashiria
hatari.
Miongozo ya utoaji elimu imeandaliwa
ikiwemo Vipeperushi. Aidha watalaamu wa Afya wanaendelea kutoa elimu kwa
wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huu kupitia vyombo mbalimbali vya
habari ili endapo ugonjwa huo ukitokea uweze kutolewa taarifa mapema
Vifaa
kinga (Personal Protective Gears) vipo vya kutosha na Wizara imeanza
kuvisambaza kutoka bohari za kanda za MSD na kuzipeleka kwenye vituo vya
kutoa huduma za afya ili watumishi wa afya waweze kutumia iwapo mgonjwa
atajitokeza. Aidha idadi itaongezwa kadiri ya mahitaji
yatakavyojitokeza.
Wizara
imebainisha vituo vya kutolea huduma kwa mikoa yote iwapo endapo ugonjwa
huu utatokea hapa nchini. Aidha katika vituo hivi, vifaa kinga pamoja
na madawa vimeshaandaliwa.
Kuwasiliana na wadau
mbalimbali ikiwemo wadau wa maendeleo ili kuweza kupata msaada wa
mahitaji mbalimbali kama yalivyoainishwa kwenye mpango wa dharura wa
kukabliana na Ebola ulioandaliwa.
Hitimisho
Wananchi
wanashauriwa kutokuwa na hofu ila kuendelea kuchukua tahadhari za
kujikinga na ugonjwa huu. Ugonjwa wa Ebola unaweza kuzuilika. Njia kuu
za kujikinga na ugonjwa huu ni:-
oKuepuka
kugusa au kuingiwa na mate, damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi na
majimaji mengine yanayotoka mwilini mwa mwenye dalili za ugonjwa wa
Ebola
oWananchi
wanatahadharishwa kuepuka kushughulikia maiti ya mtu aliyekufa akiwa na
dalili za Ebola; badala yake watoe taarifa kwa uongozi wa kituo cha
huduma za Afya kwa ushauri.
oWananchi waepuke mila na desturi zinazoweza kuchelewesha kupata huduma muhimu na kuzidi kueneza ugonjwa wa Ebola.
oZingatia usafi wa mwili tabia na kiroho.
oKutoa
taarifa mapema kwa viongozi wa Serikali na wa huduma za Afya katika
ngazi zote pale anapotokea mtu mwenye dalili za Ebola.
oKuwahi katika vituo vya huduma za Afya pale mtu anapoona dalili za ugonjwa huu.
Wizara itaendelea kushirikiana na sekta mbalimbali kuimarisha ufuatiliaji ili kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini.
Charles A. Pallangyo
Katibu Mkuu
01 August, 2014
No comments:
Post a Comment