Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 4 August 2014

PINDA: HALMASHAURI ZENYE HATI CHAFU ZIJICHUNGUZE


Na Mwandishi Wetu, Brother Danny Blog

Arusha: Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema halmashauri ambazo zimepata hati chafu kwenye miradi ya maji zinatakiwa kujichunguza.
Mhe. Pinda amesema hali ya maji nchini siyo nzuri, hivyo halmashauri hizo lazima ziwajibike kuhakikisha Watanzania wanapata maji safi na salama kupitia miradi hiyo.
Mbali ya halmashauri hizo kujichunguza, nao wakurugenzi wa halmashauri wanapaswa kuhakikisha wanaweka utaratibu wa kulinda maslahi ya umma, kwani serikali haitasita kuwachukulia hatua wakurugenzi wazembe.
Waziri Mkuu Pinda aliyasema hayo mapema leo wakati akifungua rasmi mkutano wa kujadili utekelezaji wa miradi ya maji vijijini unaoendelea kwenye Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
"Katika hili niseme tu kwamba, serikali haiwezi kusita kuwawajibisha wakurugenzi wazembe kwa sababu mwisho wa siku anayeumia ni mwananchi," alisema.
Alisema, kuna umuhimu wa halmashauri kujichunguza kwani mara nyingi uzembe wa kutokamilisha miradi hiyo unasababisha wananchi kukosa maji.
Hata hivyo, alisema kwamba kwa sasa serikali imeboresha bajeti ya maji kwa kutenga fedha nyingi, lengo likiwa kuwafikia wananchi zaidi ya milioni 10, japokuwa kwa sasa wananchi wanaopata maji ni milioni mbili tu kulingana na bajeti ya mwaka 2013/2014.
Mhe. Pinda aliongeza kwamba, jumla ya miradi 228 kati ya 240 ilitekelezwa katika mwaka huo wa fedha.
Naye Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Jumanne Maghembe, kinachokwamisha kutotekelezwa kwa miradi mingi ni baadhi ya watendaji katika sekta ya maji kushindwa kuwajibika na kutotoa taarifa kwa wakati pale penye changamoto, hali ambayo siyo makubaliano baina ya wadau wa maji na serikali.
Kutokana na hilo, aliwataka wahandisi wa maji kuhakikisha wanakuwa na taarifa muhimu kwa miradi ya maji.

No comments:

Post a Comment