Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 4 August 2014

KWA WADADA: UNATAKA TUMBO LAKO LIWE FLAT? - FANYA HIVI -1

Wanadada wengi hivi sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuwa na matumbo makubwa ama 'yaliyotepeta', tofauti na enzi zile walipokuwa wasichana. Hali hii imewafanya wengi wao wapoteze mvuto - kwao wenyewe binafsi na hata kwa wenza wao - hali ambayo inawawia vigumu kujua suluhisho.
Ni ukweli usiopingika kwamba, wanaume wengi hupoteza ama kupunguza mapenzi kwa wenza wao mara wanapobadilika kimaumbile tofauti na awali walipokuwa 'wakifukuziana'. Sababu zipo nyingi, lakini baadhi yake ni kutokana na wadada hao kujifungua ambapo tumbo haliwezi kurudi katika hali yake ya kawaida kwa urahisi.
Sababu nyingine kubwa zaidi ni kwamba wanadada wengi 'hujisahau' na kushindwa kudumisha urembo wao kama zamani. Vyakula mchanganyiko vinachangia na wengi ni wavivu wa kufanya mazoezi. Baadhi yao husema "...aah, mbona nimeshampata, sasa nidumishe urembo kwa ajili ya nini?" Hapa ndipo wanapokosea.
Unywaji wa pombe na vyakula mchanganyiko, hasa vyenye protini na hamirojo, vinachangia kubadilisha umbo la mwili, hasa mhusika anaposhindwa kuzingatia aina ya vyakula pamoja na kufanya mazoezi.
Kutokana na hali hiyo, wanadada na akina mama wengi wamekuwa wakitumia mikanda maalum ya kupunguza unene (slimming belts) kujibana matumbo yao ili yawe madogo, Wengine wanaelezwa na wataalam wa tiba mbadala kwamba wanywe maji ya uvuguvugu, na njia nyingine kadha wa kadha.
Kwa siku 21 kuanzia leo, Brother Danny Blog kwa msaada wa mtandao wa internet itakuletea vidokezo vya namna ya kupunguza tumbo na kuwa flat ili kudumisha urembo wako. Maelekezo haya yatakuja kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
Kukimbia
Kwa kuanza tu, tutawaelekeza kuhusu zoezi la kukimbia. Hili siyo lazima ulifanye kwa kukimbia barabarani au uwanjani, kama una fursa ya kwenda gym, unaweza kukimbia kwa kutumia mashine maalum (treadmills). 
Mashine hizi zimewekwa program maalum ambapo wewe mhusika ndiye unayeweza kupanga ufanye zoezi gani, ukimbie namna gani na kadhalika. Kwa hiyo unaweza kuanza kwa kukimbia (angalia hatua ya kwanza hapo chini), halafu unaweza kutembea na kukimbia (angalia maelekezo chini), na mwisho unaweza kukimbia kwa nguvu (maelekezo yako chini pia).
Zoezi hili unaweza kulifanya kwa muda wa saa 1 na dakika 39, kwa maana ya dakika 33 kwa kila hatua kati ya hizo tatu.
Kama uko Gym unaweza kumuomba mwangalizi akakuelekeza namna ya kuiseti mashine hiyo kwa kuzingatia hatua hizo tatu muhimu. Unaweza kuchapisha maelekezo hayo chini ili iwe rahisi kwako unapofanya mazoezi katika program hii.Flat-Belly Challenge Day 1: Fat-Blasting Intervals and a Slimming Smoothie

No comments:

Post a Comment