Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 2 August 2014

MISRI YAANDAA MKUTANO WA GAZA

Wapalestina waangalia mabaki ya jengo liloshambuliwa Jumamosi na Israil, kusini mwa Gaza, huko Rafah

Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi, amesema kuwa pendekezo la nchi yake la kusitisha mapigano ndio suluhu nzuri kabisa ya kumaliza umwagaji damu huko Gaza.
Rais Sisi aliwaambia waandishi wa habari kwamba hakuna suluhu nyengine mbali ya mpango wa Misri.
Waakilishi wa Marekani, Qatar na Uturuki piya wanatarajiwa kushiriki katika mazungumzo hayo ingawa haijulikani ikiwa Israil itatuma ujumbe Jumamosi.Msemaji wa Hamas alieleza kuwa ujumbe wa Wapalestina utawasaili Cairo hii leo.
Wakuu wa matibabu wa Gaza wanasema Wapalestina zaidi ya 200 wameuwawa katika mashambulio ya makomboya ya Israil tangu Ijumaa, baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kuvunjika.
Hapo awali jeshi la Israil lilisema kinga ya makombora ilizuwia makombora mawili yasifike Tel Aviv na moja lisipige Beersheba.
BBC

No comments:

Post a Comment