Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 2 August 2014

EMIRATES YAKWEPA AFRIKA MAGHARIBI

Ndege ya Emirates
Shirika la Ndege la Falme za Ghuba, Emirates, lenye makao yake Dudabi, limesimamisha kwa muda safari za ndege za kwenda Guinea kwa sababu ya ugonjwa wa Ebola ambao umeuwa zaidi ya watu 700 Afrika magharibi mwaka huu.
Katika tovuti yake Emirates imesema haiwezi kutia hatarini afya ya abiria na wafanyakazi wake.
Homa ya Ebola ilianza Guinea na kutapakaa nchi jirani za Sierra Leone na Liberia.Ijumaa, Margaret Chan, mkurugenzi wa shirika la afya duniani, WHO, alisema virusi vya Ebola vinatapakaa haraka zaidi kushinda juhudi za kuvidhibiti.
Mashirika mawili ya ndege ya Afrika, (Arik Air, ya Nigeria, na ASKY ya Togo,) yameshatangaza kuwa yamevunja safari za kwenda nchi zilizoathirika.
Shirika la ndege la Emirates halina safari za kwenda Sierra Leone au Liberia.
BBC

No comments:

Post a Comment