Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 4 August 2014

MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA WANAWAKE WATANZANIA WAJASIRIAMALI JIJINI WASHINGTON

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea shada la maua kutoka kwa Ndugu Juster Mutakyawa mara baada ya kuwasili kwenye ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Marekani iliyoko Washington
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Watanzania wanaoishi Washington kiitwacho TANO Ladies Ndugu Asha Hariz wakati alipotembelea ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kipeperushi kutoka kwa Rais na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya  Help for Underserved Communities  (HUC) ya nchini Marekani Ndugu Zawadi Sakapalla baada ya kupata taarifa ya huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo. Kampuni hiyo husaidia familia maskini kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwa kuwachimbia visima pamoja na kutoa vifaa vya elimu kwa wanafunzi.
Baada ya kutembelea maonesho ya wanawake wajasiriamali Mama Salma Kikwete akifuatana na Afisa Tawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama Lily Munanka kwenda kuweka saini kwenye kitabu cha wageni.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kwenye kitabu cha wageni. Aliyesimama kushoto ni Bibi Lily Munanka, Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka kikundi cha TANO Ladies cha nchini Marekani. Anayekabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya wanakikundi wenzake  Ndugu Juster  Mutakyawa.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akina mama wa kitanzania wajasiriamali wanaoishi nchini Marekani kwenye ukumbi wa ofisi ya ubalozi wetu mjini Washington
 Baadhi ya wanawake wajasiriamali na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akina mama wa kitanzania wajasiriamali wanaoishi nchini Marekani
 Mke wa Rais akipiga picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula.
Balozi wa Tanzania nchni Marekani Mheshimiwa Liberata  Mulamula akimuaga Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya kutembelea ofisi za ubalozi huo na kuongea na wanawake wa Tanzania wanaoishi nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment