Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 4 August 2014

WALIOKUFA KWA TETEMEKO CHINA 380

Tetemeko la ardhi nchini China
Wafanyakazi wa uokoaji nchini China wanaendelea kujitahidi kufikia eneo lililopigwa na tetemeko la ardhi katika jimbo la Yunnan siku ya Jumapili na kuua watu zaidi ya 380.
Kikosi cha dharura kinajaribu kukarabati barabara zilizoharibiwa ili kuwezesha usafiri katika maeneo yaliyopata mvua kubwa na kusababisha mmomonyoko wa ardhi.
Maelfu ya watu waliodhurika na tetemeko hilo wapo katika maeneo ambayo ni vigumu kufikiwa na mamlaka zinazohusika.
Shuhuda mmoja amesema karibu theluthi mbili ya nyumba zimeharibiwa katika kijiji chao.

Maelfu ya mahema na vitanda vya dharura vimepelekwa katika eneo hilo liloathirika na maelfu ya wafanyakazi wa idara ya dharura watumwa kusaidia kazi ya uokoaji.
BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment