Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 3 August 2014

UN YALAANI SHAMBULIO GAZA HUKU MAZUNGUMZO YAKISUSIWA

Shule ya Umoja wa Mataifa ya Rafah Gaza iliyoshambuliwa na Israil
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ameelezea shambulio la makombora karibu na shule ya Umoja wa Mataifa huko Rafah, Gaza, ambalo liliuwa watu kama 7, kuwa kitendo "kilichokiuka utu na ni cha uhalifu".
Wapalestina wanasema watu kama 10 waliuwawa.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema shambulio hilo katika mji wa Rafah, kusini mwa Gaza, lilifanywa na ndege za Israil.Bwana Ban alitoa wito mapigano yasimamishwe haraka, na kusema "wazimu huu lazima usite"
Maelfu ya raia walikuwa wanapata hifadhi katika jengo hilo.
Msemaji wa serikali ya Israel, (Mark Regev) alikanusha kuwa Israel ililenga shule yenyewe.
Nchini Israil kwenyewe mazishi yamefanywa ya mwanajeshi, Hadar Goldin, ambaye Israil ilisema awali kuwa alitekwa nyara na Hamas.
Sasa inajulikana kuwa alikufa katika mapigano.
Katika hatua nyingine, wakati ujumbe wa Palestina uko Misri kwa mazungumzo ya kusitisha mapigano, Israel inasema haitopeleka ujumbe huko.
Naibu waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Marekani, William Burns, akitarajiwa, lakini sasa inaarifiwa hatokwenda Cairo, wala mjumbe maalumu wa Mashariki ya Kati, Tony Blair.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema haikuelekea kuwa mafanikio yoyote yatapatikana katika mzungumzo hayo.
BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment