Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Sunday, 3 August 2014
UMEZIONA PETE ZA UCHUMBA ZA MASTAA HAWA?!
Hivi karibuni George Clooney alifunga uchumba na mwanasheria wa Uingereza Amal Alamuddin huku akimvisha pete kubwa ya uchumba yenye uzito wa carat 7. Mwanadada huyo akaionyesha pete yake kwa mara ya kwanza wakati alipohudhuria sherehe ya kuzaliwa ya rafiki yake Rande Gerber jijini Los Angeles mwezi Aprili. Lakini mbali ya Amal, wapo mastaa wengi ambao yawezekana pete zao za uchumba hujaziona. Hebu tazama hapa: Amal Alamuddin
George Clooney alimvisha pete mchumba wake Amal Alamuddin yenye uzito wa carat 7 ikiwa na kito cha almasi mwezi Aprili 2014.
Mwanamuziki Ciara akionyesha pete yake ya uchumba yenye uzito wa carat 15 ikiwa na kito cha almasi baada ya mchumba wake, rapa Future, kumvisha mwezi Oktoba 2013.
Mary-Kate Olsen alivalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake, Olivier Sarkozy mwezi Februari 2014 baada ya kudumu naye kwenye uchumba kwa miaka miwili, na akaionyesha mara baada ya tukio hilo alipokuwa New York na baadaye kwenye Wiki ya Maonyesho ya Mitindo jijini Paris. Chanzo: AKM-GSI na Getty
Kim Kardashian
Kanye West hakujali gharama kwa mpenzi wake Kim Kardashian wakati alipomvisha pete ya uchumba ya almasi yenye uzito wa carat 15 ambayo ilibuniwa na Lorraine Schwartz mwezi Oktoba 2013. Chanzo: Getty
Amber Heard
Amber Heard alivishwa pete ya uchumba na Johnny Depp mwezi Januari 2014.
Mila Kunis alivishwa pete na mpenzi wake wa siku nyingi na nyota wa zamani wa tamthiliya yaThat '70s Show, Ashton Kutcher, mwishoni mwa Februari 2014, tazama inavyong'ara wakati alipoionyesha kwenye mechi ya Lakers mwezi Machi.
Leighton Meester alifunga ndoa kwa siri na Adam Brody mwezi Februari 2014 lakini hakuonyesha pete yake hadi wakati wa uzinduzi wa filamu yao ya Life Partners huko Tribeca mwezi Aprili.
Nyota wa After Girls, Allison Williams alivishwa pete ya uchumba na mpenzi wake wa miaka mitatu, mwanzilishi wa kipindi cha College Humor, Ricky Van Veen, na akaionyesha pete hiyo kwenye sherehe ya baada ya tuzo za Oscar huko Vanity Fair mwaka huu.
Ginnifer Goodwin na mchezaji mwenza kwenye filamu ya Once Upon a Time, walivishana pete ya uchumba mwezi Oktoba 2013, na baadaye wakatangaza kwamba wanategemea kupata mtoto mwezi huu wa Agosti.
Miley Cyrus alivishwa pete ya uchumba na Liam Hemsworth mwezi Juni 2014. Jamaa alinunua pete yenye kito cha almasi chenye uzito wa carat 3.5 kutoka kwa Neil Lane.
Amy Adams alipigwa na mshangao wakati Darren Le Gallo alipomvisha pete ya uchumba yenye kito cha almasi chenye uzito wa carat moja ambayo imetenggenezwa na Jean Dousset. Hii ilikuwa Julai 2008.
Kate Hudson alishea kwa mara ya kwanza taarifa za uchumba wake na Matthew Bellamy mwezi Aprili 2011 wakati alipokuwa kwenye kipindi cha Today. Alionyesha pete hiyo yenye thamani ya Dola 200,000, (takriban TShs. 320 milioni), huku akisema, "Nikuwa nasubiri mtu aione."
Gabrielle Union
alitangaza uchumba wake kwa Dwyane Wade kupitia Instagram, akionyesha picha ye kidole chenye pete ya almasi. Wawili hao walionekana hadharani siku chache kabla ya Krismasi 2013.
Robin Wright alionyesha pete yake ya uchumba ya dhahabu katika tukio la Diane von Furstenberg jijini Los Angeles wakati wa tuzo za Golden Globes mwezi Januari 2014. Pete hiyo alivishwa na mwigizaji Ben Foster, ambaye walianza uhusiano wao mapema mwaka 2012.
Paris Hilton akiwa na pete yake ya uchumba yenye kito cha almasi chenye uzito wa carat 24 ambayo alivishwa na mchumba wake Paris Latsis mwezi Mei 2005. Pete hiyo ina thamani ya Dola 4.7 milioni (takiban TShs. 7.5 bilioni.
Nyota wa NBA Tony Parker alimvisha pete ya uchumba Eva Longoria mwezi Desemba 2006 ikiwa na thamani ya Dola 150,000 (TShs. 240 milioni) iliyobuniwa na Jean Dousset.
Blake Lively alionyesha pete yake ya uchumba siku ya ndoa yake na Ryan Reynolds huko South Carolina Septemba 9, 2012. Chanzo: Alex Gutierrez
Demi Moore
Demi Moore na Ashton Kutcher walikanusha uchumba wao hadi walipowafanyia suprise ndugu na jamaa zao kwa harusi yao ya siri mwezi Septemba 2005. Pete hiyo ina thamani ya Dola 250,000 (TShs. 400 milioni).
LeAnn Rimes alionyesha pete yake ya uchumba wakati wa tuzo za American Music Awards mwezi Januari 2002 aliyovishwa na mchumba wake wa wakati huo, Dean Sheremet.
Zoe Saldana, yule demu aliyecheza muvi ya Colombiana, alivishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Keith Britton mwezi Juni 2010. Lakini wawili hao hawakuweza kuoana na waliachana mwaka 2011.
Katherine Heigl akionyesha pete yake aliyovishwa na Josh Kelley mwezi Juni 2006. Pete hiyo ina kito ambacho alikichukua kwenye pete ya uchumba ya mama yake.
No comments:
Post a Comment