Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 5 August 2014

KWA WADADA: UNATAKA TUMBO LAKO LIWE FLAT? FANYA HIVI – 2

Source: Thinkstock

Vitu vinavyowavutia wanaume wengi kwa wanawake, mbali ya sura, ni umbile la mwili, hasa kuanzia kifuani kushuka chini.
Hii ina maana kwamba, kifua, tumbo, kiuno na miguu ndiyo maeneo ya kwanza kabisa kumvutia mwanamume kabla hajaangalia uso na nywele.
Lakini wanawake wengi wanatumia muda wao mwingi sana wakiwa kwenye vioo wakitengeneza nyuso zao wakijipodoa kwa angel face, lip shines, kutinda nyusi na kadhalika. Halafu wanatumia gharama kubwa kutengeneza nywele.
Mambo yote haya ni muhimu sana kwa urembo wa mwanamke, lakini kama nilivyosema jana, changamoto yao kubwa inayowakabili hivi sasa ni namna ya kutengeneza matumbo yao, au namna ya kujizuia ili wasiwe na matumbo makubwa ambayo yanaharibu shepu zao.
Wengi hawafahamu kwamba, kadili tumbo linavyokuwa kubwa ndivyo linavyoharibu muonekano. Figa ambayo ilikuwa inawapagawisha wanaume inapotea na ukifanya mchezo na tumbo hilo ukaliacha litepete, umbile lako linaweza kuwa kama boga. Yaani huwezi kujua tumbo liko wapi, kiuno kiko wapi, 'wenzele' iko wapi na kadhalika.
Matokeo yake ni kwamba, mvuto wako unapopungua, basi hata jamaa naye anapunguza mapenzi kwa sababu lile umbile la zamani lililokuwa likimpagawisha limetoweka!
Wanawake wengi wanajisahau sana hasa wanapokuwa wameingia kwenye uhusiano. Wanapenda kuwa na figa bomba lakini wanashindwa kujizuia kupanga mlo wao.
Kisingizio la kusema kwamba umezaa ndiyo maana tumbo linashindwa kurejea katika muonekano  wake wa zamani hapa hakipo kabisa. Ni uzembe tu uliopitiliza pamoja na kujisahau.
Wanawake wengi ni wavivu wa kufanya mazoezi, hata wale wanaofanya mazoezi hawazingatii kanuni zake na hujifanyia mazoezi ilimradi tu watokwe jasho.
Kama nilivyosema jana, unywaji wa pombe na vyakula mchanganyiko, hasa vyenye protini na hamirojo, vinachangia kwa kiasi kikubwa kubadilisha umbo la mwili, hasa mhusika anaposhindwa kuzingatia aina ya vyakula pamoja na kufanya mazoezi.
Wengi wamejitahidi kutumia mikanda mikanda maalum ya kupunguza unene (slimming belts) kujibana matumbo yao ili yawe madogo, lakini wapi!
Ni kwa mukhtadha huo ndiyo maana Brother Danny Blog, kwa msaada wa mtandao wa internet, inakuletea vidokezo vya namna ya kupunguza tumbo na kuwa flat ili kudumisha urembo wako. Maelekezo haya yatakuja kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza na leo ni siku ya pili ya mfululizo wa mazoezi yetu ya kupunguza unene wa tumbo.
Fanya Mazoezi kwenye Ubao (Walk the Plank)

Kufanya mazoezi kwenye ubao mpana (plank) ni moja ya mazoezi muhimu hasa ukilenga sehemu ya juu ya mwili wako.
Katika zoezi hili utatumia dakika 20 za mazoezi kwa namna sita tofauti  — kumbuka kunyoosha mgongo na mikono yako kwa dakika kadhaa baada ya kumaliza mazoezi kwenye mbao hizo.
Maelekezo ya hatua hizo sita:
Plank Mountain Climbers: Ukiwa umenyoosha mikono kwenye ubao, kunja goti lako la kulia hadi kifuani, halafu badili miguu haraka goti lako la kushoto liwe kifuani na mguu uwe kwenye nafasi ya ubao. Wengine huwa wanatumia mipira maalum kushikilia. Fanya zoezi hili kwa dakika moja.


Elbow Plank With Donkey Kick: Anza ukiwa umejikunja viwiko kwenye ubao. Kunja goti lako la kulia na kubinua kisigino chako kuelekea darini kwa sekunde 30 kama unapiga farasi-teke, kisha badili miguu.


Plank Jumping Jacks: Katika staili hii, rusha miguu yako kwa kuitenganisha na kuirejesha pamoja. Fanya zoezi hili kwa dakika moja.
Up-Down Plank: Anza kwa kunyoosha mikono kwenye ubao. Shusha kiwiko chako cha kulia chini na kisha cha kushoto, ukikaribia kidogo kwenye ubao. Kisha nyoosha mkono wako wa kulia na baadaye wa kushoto, rudi kwenye hali ya kunyoosha mikono. Rudia kwa dakika moja.
 Side Plank Leg Lift: Pumzika kwenye mkono wako wa kulia na sehemu ya pembeni ya mguu wa kulia. Nyanyua na kushusha mguu wako wa kushoto kwa sekunde 30, halafu badilisha tena mguu kwa nusu saa nyingine.
Two-Point Plank: Anza kwa kunyoosha mikono, na tanua mkono wa kulia na mguu wa kushoto. Kunja goti na kiwiko chini ya mwili wako, na kisha nyoosha. Fanya hivi kwa sekunde 30 kila upande.

Kula haya matunda

Hakika unatumia matunda hayaovernight oats katika mlo wako wa asubuhi. Yana protini nyingi na nyuzi nyuzi ambazo zinakusahaulisha njaa kwa muda. Pia yanasaidia mmeng'enyo wa chakula.Chanzo: Mtandao wa Internet

No comments:

Post a Comment