Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 5 August 2014

CHELSEA YANYUKWA 3-0 NA WERDER BREMEN DARAJANI

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
Mshambulizi wa Ivory Coast na Chelsea ya Uingereza Didier Drogba alirejea kwa kishindo Stamford Bridge lakini kuwepo kwake haikuinusuru The Blues kichapo cha mabao matatu kwa nunge (3-0 )dhidi ya klabu ya Werder Bremen ya Ujerumani.
Kipa machachari Thibaut Courtois alipewa fursa ya kushika kwenye lango huko Weserstadion.
Eljero Elia na Felix Kroos walifungia Bremen kupitia mikwaju ya penalti huku mkwaju wa kichwa kwa Ludovic Obraniak ikiisaidia timu hiyo inayoshiriki kwenye ligi ya Ujerumani Bundesliga kuandikisha ushindi.Kipa huyo mwenye umri wa miaka 22-kutoka Ubeljiji alijiunga na Chelsea mwaka wa 2011 lakini amekuwa Uhispania kwa mkopo kwa timu ya Atletico Madrid.
Elia alifunga penalti ya kwanza baada ya John Terry kuugusa mpira katika eneo la lango huku Obraniak akimsababishia aibu kipa mpya Courtois alipoiweka Bremen kifua mbele mabao 2-0 kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza.
Chelsea iliambulia kichapo cha 3-0 mikononi mwa Werder Bremen.
Licha ya mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho kumuingiza Drogba kwa mara ya kwanza tangu aiongoze timu hiyo kuilaza Bayern Munich 2012, the blues hawakuweza kujifurukuta.
Eden Hazard John Obi Mikel na Petr Cech pia walihuruhusiwa kucheza .

Toni Kroos alikamilisha kivuno hicho cha mabao alipofuma mkwaju kimiani dakika mija tu kabla ya mechi hiyo kukamilika.
BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment