Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 2 December 2014

MWANAFUNZI ALIYEKUWA ANANADI UBIKRA AKOMA, ALITOSA DAU LA DOLA 800,000

Hanna Kern, mwanafunzi aliyekuwa ananadi ubikra
Mwanafunzi anayesomea udaktari nchini Marekani ambaye alikuwa ananadi ubikra wake, amesitisha shughuli hiyo baada ya watu wachache sana kujitokeza wakiwa tayari kuulipia ubikra wa mwanamke huyo.

Pamoja na hilo Kern hakuwa na uhakika kuhusu ukweli wa waliojitokeza kulipia ubikra wake.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Dily Mail.
Mwanafunzi huyo, Hanna Kern alikuwa ananadi ubikra wake chini ya jina ambalo sio lake 'Elizabeth Raine'.
Kern ana umri wa miaka 28 na ana shahada ya uzamifu (PhD) katika chuo kikuu cha Washington, nchini Marekani.
Jarida lengine la Huffington Post, amejitambulisha kwa jina analojulikana nalo.
Kern anakuwa mwanafunzi wa hivi karibuni aliyenadi ubikra wake kwenye mtandao ambao amelazimika kuusitisha baada ya kukosa kupata kima alichokitaka na hata pia kukosa kupata wanaume wengi waliovutiwa na kampeni yake na kuhofia kuwa laiojitokeza sio watu wakweli.
Alikuliwa akisema baada ya kukosa kufanikiwa, amepata funzo na kujua kwa nini kampeni kama hizi huwa hazifanikiwi.
Wa mwisho aliyejitokeza kulipia ubikra wake alikuwa ametoa kima cha Dola 801,000, lakini mwanafunzi huyo aliamua kutoendelea na juhudi zake kwani hakufurahishwa na pesa hizo.
''Nimeamua kusitisha kampeni yangu, na kurejea katika msomo yangu ya udaktari.''
''Bado ninaamini kuwa ubikra ni kitu kizuri na pia ninaamini kuwa mwanamke anapaswa kuachwa afanye anavyotaka, ingawa masomo ndio ninayotaka kushughulika nayo kwa sasa,'' alisema Kern.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment