Marehemu Bi. Twitikege Mlagha Mafumu enzi za uhai wake.
Na Joachim Mushi
MAMA mzazi wa waandishi wa habari Kulwa, Dotto na Nico Mwaibale aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam katika Hospitali ya Hindu Mandal anatarajiwa kuzikwa leo Jumatano kijijini kwao Newland (Kibunde) Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.
Marehemu Bi. Twitikege Mlagha Mafumu ambaye ni mama mzazi wa wanahabari Kulwa Mwaibale mwandishi wa habari wa kampuni ya Global Publishers Limited, Dotto Mwaibale mwandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo na mmiliki wa mtandao wa www.habarizajamii.com na Nico Mwaibale mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) akiripotia mkoa wa Tabora alisafirishwa jana kwenda Mbeya kwa mazishi.
No comments:
Post a Comment