Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 27 December 2014

MKE WA LAURENT GBAGBO ASHTAKIWA IVORY COAST

Bi Simone Gbagbo 

Abidjan, Ivory Coast
Mke wa rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, Bi Simone Gbagbo, amefikishwa mahakamani kutokana na mashtaka ya kuhusika kwenye ghasia za baada ya uchaguzi ambapo zaidi ya watu 3,000 waliuawa.

Bi Gbagbo na watu wengine 82, akiwemo waziri mkuu wa zamani Gilbert Ake N'Gbo, wameshtakiwa kwa kuhujumu usalama wa nchi, ukabila na kwa kubuni makundi ya uhalifu.
Rais wa zamani Laurent Gbagbo, ambaye alikataa kukubali kushindwa kwenye uchaguzi mkuu miaka minne iliyopita, anasubiri kesi yake kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC) kutokana na mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Zaidi ya watu 3,000 waliuawa katika ghasia hizo baada ya rais huyo wa zamani kukataa kushindwa katika ya kura ya awamu ya pili.
Bi Gbagbo, ambaye alikuwa anazuiliwa katika kifungo cha nyumbani kwa miaka mitatu, ameshtakiwa kwa jaribio la kuhujumu usalama wa taifa hilo.
Aliyekuwa waziri mkuu Gilbert Ake N'Gbo na kiongozi wa chama cha FPI Affi N'Guessan pia wamefunguliwa mashtaka na Bi Gbagbo.
CREDIT: BBC


No comments:

Post a Comment