Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 30 December 2014

KILIMANJARO FC YAISHINDILIA POLISI KILIMANJARO 4-1, LIGI YA KILIMANJARO


Na Fadhili Athumani, Moshi
Ofisa Habari Kilimanjaro FC


HATUA ya sita bora, ligi daraja la tatu, Mkoa wa Kilimanjaro imeendelea juzi kwa mchezo mmoja ambapo Kilimanjaro FC imekurupuka kutoka usingizini na kuitandika Polisi Kilimanjaro 4-1.



Katika mchezo huo mkali uliopigwa kwenye uwanja mkali ni timu ya Kilimanjaro Polisi ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli katika dakika ya 5 tu ya kipindi kupitia kwa Bashir Malibo kabla ya Kilimanjaro FC kucharuka na kusawazisha goli dakika mbili baadae kupitia kwa Yusuph Kimanda.

Kipindi cha pili, klabu ya Kilimanjaro FC maarufu Mpira Pesa, ilirudi kwa kasi wakionesha kila dalili ya kuhitaji pointi tatu, ambapo katika dakika ya 65, Yusuph Kimanda aliongeza goli la pili na kufanya matokeo yasomeke 2-1.

Wakicheza kwa ari kubwa Kilimanjaro FC, walizima ndoto za Polisi Kilimanjaro za angalau kuchomoza na sare baada ya kupata magoli mawili ya haraka, kupitia kwa Mwinyi Juma (67) na Ayubu Lipati (87).

Kwa ushindi huo, Kilimanjaro FC imepanda hadi hadi nafasi ya tatu katika msimamo, ikiwa na pointi zake saba, nyuma ya Afro Boys yenye Pointi nane na Polisi Mwanga yenye Pointi tisa, huku Polisi Kilimanjaro ikisalia nafasi ya tano ikiwa na pointi moja.

No comments:

Post a Comment