Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 23 December 2014

MANISPAA DODOMA YAKUMBWA NA MAFURIKO

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Lephy Gembe.
Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapa, zimesababisha mafuriko katika maeneo  ya Manispaa ya Dodoma na kuzua hofu kwa wananchi ya kuibuka magonjwa ya mlipuko  kutokana na vinyesi na maji taka kuzagaa ovyo. 


Akizungumza na NIPASHE Mwenyekiti wa Mtaa wa Njedengwa Mashariki uliopo Kisasa,  Denis Said,  alisema kuwa nyumba nyingi za maeneo hayo zimejaa maji na kuzingirwa na mafuriko huku vyoo na makaro, navyo vikifurika na kusababisha vinyesi kuzagaa ovyo ndani na mitaani.

Saidi alisema kuwa wamepeleka malalamiko yao kwa mamlaka zinaozhusika kuhusiana na hali hiyo ya hatari,  lakini mpaka sasa hayajapatiwa ufumbuzi na kuzidi kuzua hofu kwa wananchi ya kukumbwa na magonjwa hayo.

“Msimu wa mvua umeanza na hizi ni mvua za pili kunyesha,  kumetokea mafuriko haya hatujui zikiendelea tutafanyaje maana maeneo mengi  wananchi wanalalamika nyumba zimejaa maji ndani vyoo na makaro ya maji taka yamefurika jambo ambalo linaweza kutusababishia magonjwa ya kuhara, ” alisema.

Alisema mafuriuko hayo yamesababisha makaro ya maji taka na vyoo kufurika na maji yake kusambaa mitaani yakiwa na vinyesi.

Alisema baadhi ya maeneo miundombinu ya barabara yake haijawahi kutengenezwa tangu wajenge makazi yao na kuziba kwa kujaa taka.

Saidi alisema ilikuwa bahati nzuri kwani mvua hizo kubwa zilinyesha juzi alfajiri na wananchi kuanza kujihami kwa kuvunja ukuta wa uzio ili kuruhusu maji kupita lasivyo, kungekuwa na maafa zaidi ya mafuriko.

Alisema kuna baadhi ya maeneo ambayo Serikali ilitengeneza barabara na kuweka lami lakini  haikuwekwa mifereji na  kusababisha maji kukosa mwelekeo hivyo kuishia  kwenye makazi yao.

Alisema  miundombinu ya barabara imeharibika hata waliotaka kwenda kwenye nyumba za kuabudu wameshindwa kwenda kutokana na magari  kushindwa kupita.

 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,  Lephy Gembe alithibitisha mafuriko kuyakumba maeneo mengi na Manispaa hiyo na kuanza kuyatembelea ili kushuhudia athari zake na kufanya tathimini.

Gembe aliyataja maeneo hayo yaliyokumbwa na mafuriko kuwa ni Makulu, Makole, Kisasa West , kisasa North, Area D na Ilazo.

Alisema  ameunda timu ya wahandisi wa ujenzi  kutoka Ofisi za Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) na Manispaa ya Dodoma  kuchunguza chanzo cha mafuriko hayo.       

 Gembe alisema wameamua kuchukua hatu hizo haraka kutokana na kuhofia kuwa huenda mvua zinazonyesha msimu huu zikawa kubwa zaidi na  kusababisha madhara zaidi ili waweze kushughulikia janga hilo kwa haraka.

 Gembe alisema timu hiyo aliyoiunda  kuna baadhi ya  eneo ilikopita imebaini kuwa mafuriko yamesababishwa na ubovu wa miundombinu.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment