Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 23 December 2014

DEREVA MANGI DEO MASENGA ATOKA NA SERENGETI KRISMASI

Displaying 1.JPG
Kaimu meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager, Elihuruma Ngowi, akiongea kwa simu ya mkononi na mshindi wa pili wa shindano la “Tutoke na Serengeti” wakati wa kuchezesha droo katika shindano la Tutoke na Serengeti ambapo, Bw. Deogratius Peter Masenga kutoka Rombo mkoani Kilimanjaro ameibuka mshindi, kulia ni mkaguzi mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Mrisho Millao. Hafla ya kuchezesha shindano hilo ilifanyika makao makuu ya Serengeti jijini Dar es Salaam.

Displaying 5.JPG
Kaimu meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager, Elihuruma Ngowi,(katikati) akiongea kwa simu ya mkononi na mshindi wa pili wa shindano la “Tutoke na Serengeti” wakati wa kuchezesha shindano hilo ambapo , Bw.Deogratius Peter, toka Rombo Kilimanjaro ameibuka mshindi, (kulia) ni mkaguzi mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Mrisho Millao na kushoto ni Meneja mwendeshaji wa kanda  Serengeti , Malalia Mmassy. Hafla ya kuchezesha shindano hilo ilifanyika makao makuu ya Serengeti jijini Dar es Salaam.

Deogratias Peter Masenga mwenye umri wa miaka 24 ambaye ni dereva wa malori makubwa na mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro atasherekea sikukuu ya krismasi kwa staili ya aina yake baada ya kuibuka mshindi wa safari inayogharamiwa na SBL kupitia kampeni yake inayojulikana kama ‘Tutoke na Serengeti’.
Deo alitangazwa mshindi katika safari ya “MTOKO WA MBUGANI” kupitia droo ya kawaida ya kila wiki iliyofanywa katika ofisi za Serengeti katika mazingira ya uwazi na kushuhudiwa na vyombo vya habari mbalimbali, Price Water Coopers (PWC) na maafisa kutoka Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa.
Akizungumza kwa njia ya simu akiwa Moshi mjini kwa shughuli zake za kikazi, Bw, Deo ambaye alijawa na bashasha mara baada ya kupata taarifa hizo alisema “Hii ni mara yake ya kwanza kushinda kitu cha namna hii. Nina furaha sana kuibuka mshindi, hakika naumaliza mwaka kwa staili ya aina yake nawashukuru sana Serengeti”. 
Deo ambaye alimchagua kaka yake kama mtu wa kwenda naye kwenye safari hiyo, aliwashauri watu wengine wasikate tamaa na kujaribu kushiriki mara kwa mara katika promosheni hii . 
Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Bia ya Serengeti, Bw. Elihuruma Ngowi alisema ...”Kampuni ya Serengeti itatumia kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 10 kwa ajili ya safari ya mshindi na anaruhusiwa kwenda na mwenza au mtu yeyote atakaye mpendekeza kwenye mtoko huu wa siku mbili katika mbuga ya wanyama ya Serengeti.... Kiasi kilichotajwa kitawawezesha kupata fedha za kujikimu, malazi, usafiri na mambo mengine,” aliongeza Elihuruma Bw. Elihuruma alisisitiza kwamba promosheni hiyo bado inaendelea na milango ipo wazi kwa wateja wote na kuwaomba waendelee kujitokeza kushiriki “Bado kuna washindi watatu watakaoshinda safari hii ya Serengeti, kwa hiyo nachukua fursa hii kuwatia moyo wateja wote wa Serengeti kuendelea kushiriki kwenye promosheni hii ya aina yake”. 

Ili kuweza kushiriki kwenye promosheni hii wateja wanatakiwa kununua bia ya Serengeti Premium Lager na kuangalia ndani ya vizibo na kuna namba ambazo wanapaswa kuzituma kupitia ujumbe wa simu za mkononi (sms) kwenda 15317 na moja kwa moja wataingia kwenye droo na kuweza kushida zawadi kama vile Limo Bajaj, Pesa Taslimu, Punguzo la shilingi 300 kwenye bia na bia za bure na unavyozidi kutuma namba hizo kutoka kwenye vizibo ndipo unapojihakikishia nafasi ya kushida.

No comments:

Post a Comment