Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 27 December 2014

WALIMU KENYA KUANZA MGOMO JANUARI 5

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Kenya (KNUT) Wilson Sossion

Nairobi, Kenya
CHAMA cha Walimu Kenya (KNUT) kimeitisha mgomo nchi nzima wa walimu kuanzia Januari 5, kikieleza kwamba mazongumzo yao na Tume ya Utumishi wa Walimu kuhusu maslahi yao hayakuzaa matunda.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Sossion ametoa notisi ya siku saba kwa Wizara ya Ajira pamoja na TSC kabla ya kuanza rasmi kwa mgomo huo.
Chama hicho kimewataka wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari kutokwenda shule kuanzia Januari 5 wakati watakapoanza mgomo huo.
Chama hicho kimeilaumu Tume ya Mishahara kwa kukaidi kuboresha mishahara ya walimu pamoja na mazingira yao ya kazi.
Sossion alisema: “Tume ya mishahara haijatengua waraka wake wa kuongeza posho kwa mawaziri na makatibu wakuu.”
Waraka huo uliongesza posho kwa mawaziri hadi KShs. 200,000 kwa mwezi na kwa makatibu wakuu ni KShs. 150,000 kuanzia Januari Mosi, 2015 waraka ambao chama hicho kilitaka utenguliwe kufikia Jumatano iliyopita.
Sossion aliitaka serikali kujiandaa na mgomo huo wa walimu nchi nzima na kwamba hawatarudi nyuma.



No comments:

Post a Comment